HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 01, 2023

UZINDUZI WA HAMASA NI UNYAMA MWINGI

Na John Marwa

Klabu ya Simba imezindua hamasa kuelekea kilele cha wiki ya Simba ambapo kitahitimishwa Agosti 6 Uwanja wa Benjamin Mkapa na siku ya wanasimba.


Simba Day Unyama Mwingi itafanyika Agosti 6 mwaka huu, ukiwa ni mwaka wa 14 wa tamasha hilo kubwa la michezo Barani Afrika ambalo hutumika kuwakutanisha wanasimba na kuwatambulisha wachezaji wao wa msimu mpya.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa hamasa uliofanyika Buza jijini Dar es Salaam kuelekea kilele cha Simba Day Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo Ahmed Ally amewataka wapenzi na mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi kwani ndio utaratibu wao linapokuja jambo lao.

"Tumekuwa na utaratibu wa kupita eneo kwa eneo ili kuwafikia Wanasimba, kuwe kuna mabonde, milima ilimradi Wanasimba wenzetu wapo sisi tutafika ndio maana leo tupo hapa Buza. Lengo letu ni kuhakikisha tunawaalika Wanasimba mjitokeze kwa wingi kwa Mkapa siku ya Jumapili.”- Ahmed Ally ameongeza kuwa.

"Kuna mchezaji kila dirisha la usajili likifunguliwa wanamsajili lakini msimu ukianza anachezea Simba, njoo Jumapili kwa Mkapa mje mumwone." Amesema Ahmed.

Wapenzi mashabiki na wanachama wamejitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo, jambo linalotoa ishara njema kuelekea kilele cha Simba Day.



No comments:

Post a Comment

Pages