Na John Marwa
Wananchi, Yanga SC wameepiga shagwe la kutosha jioni ya leo katika Dimba la Azam Complex Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam katika mchezo, wa awali Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL dhidi ya Asas ya Djibouti kwa kuwanyeshea mvua ya mabao (5-1).
Ulikuwa mchezo wa pili wa hatua ya awali kutinga hatua ya kwanza ya mashindano hayo kuwania kutinga hatua ya Makundi CAF CL.
Mchezo huo waliupatia jina la nyota wao Max Nzigeli kwa mtindo wake wa kucheza akiwa amechomekea, 'Max Day' ambapo mashabiki waliojitokeza walitekeleza kwa vitendo.
Yanga wamepata mabao yao kupitia kwa Max Nzigeli aliyefunga mabao mawili, Pacome, Konkoni na Mzize. Wakati Asas wakipata bao la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati uliowekwa kimiani na Tito.
Mchezo wa kwanza ambao Asas walikuwa nyumbani walipoteza kwa mabao mawili kwa bila. Kipigo cha mabao (5-1) kinawafanya kuondoshwa kwa jumla ya mabao (7-1).
Ushindi huo unawafanya Yanga kukutana na El Merreikh ya Sudan, ambapo dakika 180 zitaamua nani kutinga hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL 2023/24.
August 26, 2023
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.



No comments:
Post a Comment