Na Magrethy Katengu
Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko aliagiza Shirika la Umeme Tanesco kuhakikisha Watanzania wote wanafikiwa na huduma ya Umeme kuanzia Mijini hadi vijijini ili kusaidia shughuli za kiuchumi kuendelea.
Agizo hilo amelitoa leo Jijini Dar es salaam katika kikao cha Wafanyakazi wa Tanesco kutoka kila Mkoa ambapo amesema jitihada za makusudi lazima zifanyike ili kila mahali umeme ufike kwani watanzani wao hawana maneno mengi isipokuwa kero yao kubwa ni suala la kukatika katika umeme inasababisha shughuli zao za kiuchumi kudhorota
“Watanzania wanataka umeme hawataki maneno umeme ukiwepo wa uhakika na haukatiki katikikatiki huwezi ukasikia Shirika la Umeme likilaumiwa kama nyinyi hamjashirikiana kuacha kulinda vyeo vyenu mkaka na kushungulikia suala Moja tu upatikanaji wa umeme wa uhakika mtafanikiwa kwa kiasi kikubwa tuache kushughulika na Matatizo ya wafanyakazi '' amesisitiza Naibu Waziri Mkuu
Hata hivyo Dkt Doto amesisitiza kuunganisha wafanyakazi ambao ndiyo raslimali watu na Viongozi wasiwavunje moyo kwa kuwagawanya makundi makundi wawaone wote ni sawa mbele ya macho yao ili hata wanapotoka majumbani mwao watamani kuja kazini na lengo lililokusudiwa likamilike Upatikanaji umeme wa uhakika kwa Watanzania wote.
"Kupendana kushukamana pasipokujali vyeo, kuthaminiana ni nguzo pekee kazini kwani kila mmoja ana mchango katika kufikia lengo lililokusudiwa acheni maneno maneno yanayopelekea kuleta makwazo shughulilieni suala Moja acheni kushughulika na watu tambueni majukumu. yenu kila. mmoja afanye kazi kwa bidii" amesisitiza
Naibu Waziri Mkuu Dkt BitekoTaasisi nyingine za Serikali moja ya mambo tunayotakiwa kufanya ni kuzingaunisha taasisi nyingine ikiwemo REA TPDC kwani zote hizi hutegemeana na Waziri wake ni mmoja ili tuweze kuwafikia watanzania kwa haraka, na kazi hii ni ya kwetu.
Sanjari n hayo nawaonya viongozi mahali pa kazi patakuwa pagumu kama mtakuwa mmekusanya genge la soga na wapiga majungu kazini, na mwisho watanzania hawatapata umeme, wafanyeni watu hao kuwa ni daraja linalofanana na kama tutashughulika na masuala binafsi ya watu badala ya masuala ya kazi hamtafikia malengo kwani kuna watu wanahofu ya mabadiliko, na hali hiyo tunaitengeneza sisi viongozi, kwa sababu ukiingia mahali badala ya kushughulika na jambo unaanza kushughulika na watu, na wafanyakazi wote hawa maisha yao yote ya utumishi wao masaa mengi wanatumia wakiwa kazini, hawa ni binaadamu, kuna wakati watakuwa wamekwazwa, wamevunjika moyo msikimbilie kuwasimamisha kazi kaeni nao chini ujue tatizo lake na ujue siyo kutoa maamuzi magumu wengine ni wagonjwa.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba amemuhakikishia Naibu Waziri Mkuu Dkt. Biteko kuwa Wizara yake kupitia shirika la TANESCO imekuwa ikifanya mikakati na kila jitihada za kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora na za uhakika za Nishati ya Umeme.
No comments:
Post a Comment