HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 01, 2023

JUKATA ; MIAKA MITATU KUTOA ELIMU YA KATIBA NI UCHELEWESHAJI WA UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA

 Na Magrethy Katengu


Jukwaa la Katiba Tanzania JUKATA limeishauri  Serikali kuanchana na Mpango wa kutoa Elimu ya Katiba ya mwaka 1977 kwa miaka mitatu kama ilivyotoa msimamo huo kupitia aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damasi Ndumbalo badala yake ipeleke miswada ya Sheria za michakato wa katiba katika tume ya wataalamu itakayoundwa kwa ajili ya marekebisho na upatikanaji wa katika mpya 



Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa JUKATA Bob Chacha Wangwe amesema ni vyema serikali kuona umuhimu wa kutumia nyaraka muhimu za ya mchakato wa katiba katika kutunga au kurekebisha Sheria za mchakato wa katiba kwakuwa zimezingatia mahitaji ya Sasa ya nchi pamoja uziefu wa mchakato uliokwama 2014.


"Tunatoa wito kwa Waziri wa katiba na Sheria Balozi Dkt Pindi Chana kutoa mapema ratiba za hatua za mchakato wa katiba mpya ili kuondoa sintofahamu ambayo imetawala miongoni mwa Watanzania na wadau mbalimbali kwa ujumla " amesema Bob Wangwe


Aidha amesema kuwa  Jukata bado linaamini hatua iliyotangazwa na wizara ya Katiba na sheria hivi karibuni ya kutoa Elimu ya katiba  ya mwaka 1977 kwa miaka mitatu ni hatua ambayo inatakiwa kuangaliwa upya kwani ni ucheleweshwaji wa kuanzisha mchakato wa katiba na kutumia vibaya fadha za watanzania kwani hatua hiyo ilishafanyaika na iliyokuwa.tume ya marekebisho ya katiba mwaka 2014  .


" Ujio wa Balozi Dkt  Pindi Chana katika Wizara ya Katiba na sheria tunaamini utaleta Nuru mpya yenye mwangaza  ya upatikanaji wa katiba mpya  na kuondoa vikwazo ambavyo kwa namna moja ama nyingine vitaweza kutukwisha kama hilo la kutoa elimu ya Katiba ya mwaka 1977 kwa miaka mitatu " amesema Bob


Nakuongeza kuwa" JUKATA tunampongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kumuondoa Dkt Damasi Ndumbaro kwenye Wizara ya Katiba na Sheria kwani tunaamini aliona atachelewesha baadhi ya kazi na  hivyo na kutafuta mtu mwingine kwa ajili ya kumsaidia kumsaidia Wizara hivyo sisi kama wananchi  tunaahidi kumpa Ushirikiani lakini pia kumtakia kila la  kheri katika majukumu yake mapya " amesema Bob Wangwe



Awali akizungumza Mwenyekiti wa Jukata Dkt  Ananillea Nkya amesema Mchakato wa upatikanaji katiba mpaya unatakiwa ufanyike haraka  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kutengeneza Sheria  mfano  ili watanzania wote wajue namna ya kupata katiba mpya .


Dkt Nkya amewaomba watanzania kuwa kitu kimoja katika kupata  katiba mpya kwakuwa jambo hilo halihitaji kuwa na utashi wa kisiasa hivyo linahitaji Uzalendo maslahi mapana ya kitaifa.


Naye Mjumbe wa bodi ya Jukata Deus Kibamba  amesema Mchakato huo utaendelea  pale upoishia   kwa kufuata rasimu ya katiba ya Jaji Warioba kwa kuipeleka kwa wananchi waendelee kutoa maoni yao kabla ya kupelekwa kwa Mamlaka husika  kwa ajili ya ukamilishaji wa katiba Mpya 

Aidha Jukata wameshatengeneza Sheria mfano zinazoweza kutumika na tume ya wataalamu katika upatikanaji wa katiba mpya. 

No comments:

Post a Comment

Pages