Na Victor Masangu, Kibaha
Mbunge
wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ametekeleza ahadi yake kwa
vitendo kwa wafanyabiashara wa soko la mnalani kwa kuwakabidhi matenki
makubwa matatu kwa ajili ya kuhifadhia maji.
Koka
amekabidhi matanki hayo wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la
kuweza kuwatembelea na kuzungumza na wafanyabiashara wa bidhaa mbali
mbali ikiwa sambamba na kutekeleza ahadi zake ambazo aliziahidi kipindi
cha nyuma.
Aidha katika
ziara hiyo Mbunge Koka ambaye aliambatana na viongozi mbali mbali wa
chama pamoja na viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha
Nikson Saimon pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Kibaha Mussa
Ndomba.
Mbunge huyo
alisema kwamba ana imani kwamba matanki hayo ya maji yataweza
kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kero na adha ambayo ilikuwa
ikiwakabili wafanyabiashara hao kwa kipindi cha muda mrefu.
Sambamba
na hilo Koka amekabidhi televisheni (TV) mbili za kisasa zenye ukunbwa
wa nchi 45 kwa lengo la kuwapa guess ya wafanyabiashara hao kutazama
na kupata matukio na taarifa mbali mbali kutoka ndani na nje ya
nchi.
"Kipindi cha nyuma
nilipita katika soko hili na niliahidi matanki ya maji makubwa
matatu.,Televisheni mbili sambamba na vifaa vya michezo ikiwemo mipira
pamoja na jezi na leo hii nimekuja rasmi kwa ajili ya
kuvikabidhi,alisema Koka.
Aidha
Mbunge huyo aliongeza kwamba lengo lake kubwa ni kuwawekea mazingira
mazuri wafanyabiashara hao ili soko liweze kuwa la kisasa zaidi na
waweze kufanya biashara zao katika mazingira ambayo ni rafiki.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nikson Saimon alimshukuru kwa
dhati Mbunge huyo kwa kuweza kuona umuhimu wa kuwasaidia wafanyabiashara
hao na kwamba serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuendelea
kuboresha miundombinu ya soko hilo.
Naye
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Kibaha Mussa Ndomba alibainisha kuwa
kwa sasa wameshatenga zaidi ya milioni 200 kwa ajili ya kuezeka paaa
katika soko hilo ili kuondokana na changamoto hasa katika kipindi cha
mvua kwani bidhaa zimekuwa zikilowa.
Nao
baadhi ya wafanyabiashara katika soko hilo wamempongeza Mbunge huyo kwa
kuweza kutekeleza ahadi yake kwa vitendo na kwamba matanki ya maji
waliyopatiwa yatakuwa ni mkombozi mkubwa wa upande wao katika kuhifadhi
maji.
No comments:
Post a Comment