Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus akizungumza na Viongozi pamoja na Wahariri kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari kuhusiana na Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF-Afrika Food Systems Summit 2023), Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Septemba, 2023.Wahariri pamoja na Viongozi mbalimbali waliohudhuria Kikao kuhusu Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF-Afrika Food Systems Summit 2023) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Septemba, 2023. Mkutano huo wa Chakula unatarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 05 -8 Septemba 2023.
Na Suleiman Msuya
ZAIDI ya watu 3,000 kutoka nchi 70 dunini wanarajiwa kushiriki katika mkutano wa siku nne wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF), unaotarajiwa kuanza Septemba 5 hadi 8 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus wakati akizungumza na waandishi Ikulu jijini Dar es Salaam leo, ambapo amesema mkutano huo unafanyika kutokana na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kuomba ufanyike nchi.
Amesema mkutano huo utakutananisha watu wa kada mbalimbali kama viongozi wa nchi, watu maalum, vijana, watalaam wa kilimo, watunga sera, wafanyabiashara, wawekezaji, watunga sera, wakulima, wafugaji na wavuvi kutoka kila kona ya dunia.
Yunus amesema hadi sasa zaidi ya watu 3,000 kutoka nchi 70 wamethibitisha kushiriki, hivyo ni matumaini ya Serikali kuwa mkutano huo utakuwa na matokeo chanya.
“Desemba 12, 2022 Rais Samia alihudhuria mkutano wa AGRF ambao ulifanyika nchini Senegali, ambapo alitumia nafasi hiyo kuomba Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka huu na tulikubaliwa kutokana na jitihada za Serikali kutenga bajeti kubwa katika sekta ya kilimo,” amesema.
Yunus amesema mkutano huo wa AGRF umewahi kufanyika Tanzania mwaka 2012, hivyo ni jambo la faraja kupata fursa hiyo kwa mara nyingine nan i ushahidi tosha kuwa Serikali imeweka mkazo katika sekta ya kilimo, ufugaji na uvivi.
Amesema mkutano huo utawezesha wahusika kujadili kwa kina namna ya kusimamia mifumo ya chakula Afrika na duniani kwa ujumla, hiyo ikitokana na ukweli kuwa chakula ni muhimu kwa kila kiumbe.
Mkurugenzi huyo amesema kupitia mkutano huo Tanzania itaweza kutangaza fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya kilimo, uvuvi, mifugo na utalii ambazo zina mchango mkubwa katika pato la taifa.
Yunus amesema taarifa za sasa zinaonesha Tanzania ina ng’ombe zaidi ya milioni 36.6, mbuzi milioni 26, kondoo 6.1, kuku milioni 97.4 na samaki katika Ziwa Victoria inadaiwa kuna akiba zaidi ya tani milioni 2.23.
“Pia jukwaa hili la kimataifa litatoa fursa za kujadiliana kwenye eneo la uchumi wa buluu, kilimo cha mwani na mengine ambayo yana mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi,” amesema.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo amesema mkutano huo utarajiwa kushirikisha marais saba, mawaziri wakuu na wawakilishi wan chi zote 70
Balozi huyo amesema mkutano huo utachangia ukuaji wa uchumi, kutokana na shughuli ambazo zitafanyika kwa siku tano.
Amesema idadi ya washiriki wataweza kutumia bidhaa za Tanzania kama vyakula, maji, vinywaji na malazi, hali ambayo itawezesha nchi kuingiza fedha za kigeni.
Balozi Shelukindo amesema Rais Samia aliagiza wizara hiyo na nyingine kuhakikisha Tanzania inakuza utalii wa mikutano na AGRF ni mwendelezo wa mkutano wa Rasilimali Watu ambao ulifanyika mwezi Julai mwaka huu JNICC.
Katibu huyo amesema mwezi ujao mawaziri wamiundombinu kutoka nchi Afrika wanatarajiwa kukutana Kisiwani Zanzibar, hivyo ni ushahidi tosha kuwa nchi imefunguka.
No comments:
Post a Comment