NA DENIS MLOWE ,IRINGA
MKOA wa Iringa
unatarajia kuwa na kiwanja Cha kisasa Cha mchezo wa Golf kinachoendelea
kujengwa na Mkwawa Golf Club katika eneo la Kihesa Kilolo.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa kiwanja hicho Mwenyekiti wa Mkwawa Golf Club,
Edmund Mkwawa alisema kuwa ujenzi wa uwanja huo utagharimu kiasi Cha
milioni 200 na kutakuwa na viwanja 9 vya gofu kwenye eneo la hekta 30.
Mkwawa
alisema mchezo wa Golf ni burudani inayovutia sana watalii hasa
ikizingatiwa Mkoa huo ni lango kuu la utalii katika ukanda wa Nyanda za
Juu Kusini.
Mkwawa alisema uwanja huo licha ya kuwa na viwanja 9 kutakuwa na Hotel ambapo itaendelea kuchechemua Utalii kwa mkoa Kusini.
Alisema
kuwa mchezo wa Golf unapendwa na watu wengi sana hivyo kitendo Cha
kutengeneza katika viwanja wa utalii itakuwa Moja ya chafu ya kupata
watalii.
Mkwawa alisema kuwa
kila kitu kimekamilika kilichobaki ni ujenzi wa uwanja huo ambapo
kutakuwa na kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya mchezo wa Gofu.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Veronica Kessy alisema kuwa ni
vyema wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa
kutangaza vivutio hivyo vya utalii vilivyopo katika mkoani hapa
kutokana na upekee wa vivutio hivyo.
Alisema
kuuwa vivutio vya Utalii ambavyo ni vizuri na vya Kipekee
vinavyopatikana katika Mikoa ya Kusini mwa Tanzania ni fursa kwa
Wananchi wa Mikoa hiyo kunufaika na kujiongezea kipato kutokana na uwepo
wa vivutio hivyo.
Aliongeza kuwa ujenzi wa
uwanja huo utakuwa ni Moja ya maeneo yatakayovutia watalii kwani mchezo
mingi huwaleta watu karibu hivyo golfu ni Mmoja ya michezo ambayo jamii
ya wageni wanapenda kucheza.
Naye mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu alisema uwanja huo ni chachu ya kukuza utalii Nyanda za Juu Kusini
Aliongeza
kuwa uwanja huo ambao utajengwa mkoani hapa itasaidia kukuza vipaji ya
watoto katika mchezo wa Golf hivyo kuwa na Wacheza wengi zaidi hapo
mbele.
No comments:
Post a Comment