Makamu
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa
Mohamed Ali Kawaida amemtaka Katibu Mkuu wa Umoja huo Fakii Raphael
Lulandala kuhakikisha analeta mabadiliko ya kiutendaji.
Kawaida
ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam akizungumza katika hafla ya
mapokezi ya Katibu Mkuu huyo mpya aliyeteuliwa hivi karibuni
yaliyofanyika jijini humo.
"Taasisi
imepata Mtendaji Mkuu na alishapokelewa na watendaji wenzake Makao
Makuu Dodoma na sasa yupo tayari kwa kuanza rasmi kazi za UVCCM, tuna
mpango kazi wetu wa miaka mitano na miaka mitatu," amesema Kawaida na
kuongeza,
"Tuna
Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi iliyojielekeza kuhakikisha
tunapambania maslahi ya vijana, hivyo unapaswa kuhakikisha hilo
linatimia,".
Hivyo
Kawaida amebainisha Kama Mtendaji Mkuu wa UVCCM Taifa anapaswa
kuhakikisha anawasimamia Watendaji wengine wote katika ngazi mbalimbali
ikiwemo wa mikoa na Wilaya ili kufanya Umoja huo uzidi kuimarika
kiutendaji nchi nzima.
Amesema
kwamba mabadiliko ndani ya UVCCM hataweza kuyafanikisha pasipo na
ushirikiano na watendaji wengine, hivyo ametakiwa kushirikiana nao bega
kwa bega.
Kawaida
amemwagiza pia kuhakikisha Idara ya Chipukizi inakuwa imara kwa
kuhakikisha anakuja na mpango wa Wiki ya Chipukizi ambayo Chipukizi
wataitumia kuwasilisha changamoto zao na maoni yao kwa maendeleo ya
chama.
Kadhalika
Kawaida amemtaka Katibu Mkuu huyo kuandaa mpango wa kushugulikia kero
za vijana ambao ni Wakulima, wanafunzi, wajasiriamali, wavuvi,
wachimbaji wadogo wadogo na kadhalika ili kupigania maslahi yao na
kuwainua kiuchumi.
"Hivyo tushughulike na makundi haya na kushughulikia changamoto zao," ameeleza Kawaida.
Vile vile Kwaida amemuelekeza Katibu Mkuu kuandaa mpango kazi wa kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi juu ya vijana.
Kwa
upande wake, Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Rehema Sombi amesema
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mengi na makubwa ikiwemo
kuwawezesha vijana kwa kiasi kikubwa kwani amewatoa mtaani na kuwapeleka
saiti kwenye kilimo, ajira, mikopo kutoka mfuko wa uwezeshaji na
kadhalika.
Aidha
ameeleza kuwa baada ya miezi minne kupita bila safu ya uongozi wa UVCCM
Taifa kukamilika, sasa imekamilika baada ya uteuzi wa Katibu Mkuu huyo
Lulandala.
No comments:
Post a Comment