Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwatunuku Digrii za Awali, Stashahada na Ashtahada kwa wahitimu 2796 katika Mahafali ya 53 ya duru la pili la chuo hicho yaliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam leo Jumanne Oktoba 17, 2023.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na wahitimu Elizabeth B. Kway na Placidi Leonardi Lala, wahitimu wa shahada ya awali ambao wamefaulu daraja la kwanza kwa wakia (GPA) ya 4.8 ambao ni ufaulu wa juu kupita wahitimu wote 2796 katika Mahafali ya 53 ya duru la pili la chuo hicho yaliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam leo Jumanne Oktoba 17, 2023. Bi. Kway amefuzu Digrii ya Awali ya Sayansi katika Sayansi za Takwimu Bima (Bachelor of Science in Acturial Sciences) wakati Bw. Lala amefuzu Digrii ya Awali ya Elimu Jamii katika Muziki (Bachelor of Arts in Music).
No comments:
Post a Comment