Na Lydia Lugakila Kyerwa.
ASKARI wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wamefanikiwa kuyaondoa makundi ya wanyamapori aina ya Tembo walikuwa wamevamia maeneo ya vijiji vitano vilivyoko kwenye kata ya businde iliyoko wilayani kyerwa Mkoani Kagera kwa zaidi ya miaka 10 na kusababisa kaya zaidi ya 50 kuhama katika vijiji hivyo kwa hofu ya wanyama hao walioanza kuwashambulia na kuwaua pamoja na kuharibu mazao yao ya kilimo mashambani.
Kamishina wa Uhifadhi Dkt. Fredrick Mofulu ambaye ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ibanda-Kyerwa iliyoko wilayani kyerwa mkoani humo aliyeongoza operesheni hiyo alisema ilichukua siku tano hadi kufanikiwa.
Alisema vijiji vilivyokuwa vimevamiwa na tembo hao viko kwenye kata ya Bisinde ambavyo ni Nyakashenyi, Businde, Kibare, Bugara na Kijumbura , alieleza kuwa tembo hao wamedhibitiwa na kuswagwa hadi kwenye umbali wa kilomita zaidi 45 kutoka katika maeneo ya vijiji hivyo yaliyokuwa yamevamiwa.
Kamishina huyo alisema tembo hao wameishadhibitiwa na anayo matumaini ya kuwa hawatarudi katika vijiji hivyo kwa njia za kuingia alizosema kuwa ni tatu zimeishabainika na zitawekewa ulinzi wa kutosha utakaowazuia kupenya.
Alisema katika kuimarisha ulinzi wa kuwadhibiti tembo wasirudi katika vijiji hivyo umeanzishwa mpango wa kutoa mafunzo kwa vijana wa vijiji hivyo ya namna ya kuwadhibiti tembo hao yatayotolewa na chuo cha wanyamapori cha Pasiasi kilichoko mkoani Mwanza.
Aliendelea kusema kuwa mafunzo hayo yatawajengea uwezo mkubwa vijana hao wa kupata mbinu za kitaalam za kuwadhibiti tembo wasirudi tena katika maeneo ya vijiji, na kila kijiji kitatoa vijana 2 ambao watapata mafunzo hayo.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Bi. Zaitun Msofe alishukuru kazi kubwa iliyofanywa na askari wa TANAPA ya kuwaondoa tembo hao ambao walishakuwa kero kubwa kwa Wananchi ya aVijiji hivyo.
“Wengi wamejaribu wameshindwa lakini nyie mmeweza, nawashukuru sana Wananchi wangu wataishi kwa amani na utulivu, walikuwa wamekata tamaa, sasa nawataka mfanye kazi mpunguze maumivu mliyokuwa mnayapata baada ya kuvamia na tembo" alisema Bi Msofe.
Aliahidi kuwa serikali ya awamu ya sita itaendelea kutatua kero zao zikiwemo za ukarabati wa barabara na kuchimba visima vya maji na pia itaendelea pia kutatua kero zinazosababishwa na Wanyama waharibifu wakiwemo Viboko wanaosumbua na kushambulia watu katika eneo la Kakanja lililoko wilayani Kyerwa.
Nao baadhi ya Wananchi waliolazimika kuhama vijiji vyao kwa hofu ya kushambuliwa na tembo wakizungumza kwa nyakati tofauti waliishukuru serikali kwa kumaliza tatizo hilo na wameahidi kurudi kwenye maeneo yao kuendelea na shughuli zao baada ya kuhakikishiwa usalama wa maisha yao na mali zao.
November 30, 2023
Home
Unlabelled
ASKARI TANAPA WAFANIKIWA KUWAONDOA TEMBO WALIOKUWA WAMEVAMIA VIJIJI 5
ASKARI TANAPA WAFANIKIWA KUWAONDOA TEMBO WALIOKUWA WAMEVAMIA VIJIJI 5
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment