Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule (wa tatu kushoto), akipokea sehemu ya msaada wa viti na meza 5o kutoka kwa Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd (wa tatu kulia) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, Mkuu wa Shule ya Sekondari Bunju 'A' Bupe Mkondola (wa pili kushoto), Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Kinondoni, Beatrice Bangesi (kulia), Meneja Mwandamizi Idara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Benki ya CRDB, Suzan Shuma (wa pili kulia).
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule (wa pili kushoto) na Mkuu wa Shule
ya Sekondari Bunju 'A' Bupe Mkondola (kulia) wakisaini nyaraka baada ya
kupokea msaada wa viti na meza 50 kutoka Benki ya CRDB. Wa pili kulia ni
Meneja wa Benki ya CRDB kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd akishuhudia.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya viti na meza 50 kutoka Benki ya CRDB kwa ajili ya Shule ya Sekondari Bunju 'A'.
Meneja wa Benki
ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd (wa pili kulia), akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum Janeth Mhawanga, katika hafla ya makabidhiano ya viti na meza 50 kwa Shule ya Seko ndari Bunju 'A', kulia ni Meneja Mwandamizi Idara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Benki ya
CRDB, Suzan Shuma na kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la CRDB Kinondoni, Beatrice Bangesi.
No comments:
Post a Comment