HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 23, 2023

UCSAF: Bilioni 326 kuwezesha upatikanaji wa mawasiliano ya uhakika maeneo ya vijijini

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba, akiwasilisha Ripoti ya Utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo kwenye kikao kazi kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kilichofanyika jijini Dar es Salaam.



Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Deodatus Balile akizungumza wakati wa Kikao Kazi kilichoandaliwa na Ofisi ya Hazina jijini Dar es Salaam.



Na Mwandishi Wetu

 
Serikali kupitia mfuko wake wa mawasiliano kwa wote (UCSAF), imesema wananchi zaidi ya milioni 23 watapata huduma ya mawasiliano ya Simu kwa uhakika, baada ya kukamilika kwa mradi wa Ujenzi wa Minara 2,149 kwenye maeneo ya Vijijini, ambapo kiasi cha Shilingi Bilioni 326 zitatumika.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba, ametoa kauli hiyo leo Novemba 21, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha Ripoti ya Utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo kwenye kikao kazi kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

"UCSAF kama taasisi ya Serikali  imeingia makubaliano ya Kimkata na watoa huduma ya Mawasiliano ili kufikisha huduma hiyo kwenye kata 1,974 zenye Vijiji 5,111, ambapo mpaka sasa Jumla ya Kata 1,197 zenye Vijiji 3,613 huduma hiyo ya mawasiliano imekwisha fika kwenye maeneo hayo" amesema  Bi Justina.

Kuhusu mradi wa Tiba mtandao Afisa Mtendaji Mkuu huyo amesema UCSAF inatekeleza kwa Kushirikiana na Taasisi ya DIT, Hospitali ya Muhimbili, Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Milango ya Fahamu (MOI) pamoja na Hospitali zingine kubwa hapa nchini.

"Hospitali zilizounganishwa mpaka sasa ni Hospitali ya mkoa wa Morogoro, wakati hospitali ambazo zipo kwenye hatua ya kukamilishwa ni pamoja na Hospitali ya mkoa wa Ruvuma, Tanga pamoja na Katavi" ameeleza Bi Justina Mashiba.

No comments:

Post a Comment

Pages