HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 11, 2023

DC MSOFE AKEMEA VIONGOZI WANAOINGILIANA KI MAJUKUMU

Na Lydia Lugakila

Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Zaitun Msofe amekemea vikali tabia ya baadhi ya viongozi wanaoingilia majukumu ya watendaji kuanzia ngazi ya kijiji na kusababisha kushindwa kutimiza majukumu yao kwa ufanisi na kwa wakati.

Msofe ametoa kauli wakati akitoa maelekezo ya serikali katika kikao cha Baraza la Madiwani kwa robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 katika Halmshauri ya wilaya ya Kyerwa likichofanyika Novemba 10, 2023 katika ukumbi wa Rweru Plaza ulioko katika Wilaya humo.

 Mkuu wa Wilaya hiyo amesema kila mmoja anapaswa kubaki katika misingi ya kazi yake na sio kuingilia majukumu ya mtu yoyote ili kuepusha migogoro katika utendaji kazi.

Msofe amesema kuwa ni jukumu la watendaji wote kuanzia ngazi ngazi ya kijiji kufanya kazi kwa kuzingatia sheria kanuni taratibu na miongozo iliyopo.

"Tusifanye kazi kwa kufuata utashi wetu, wala utashi wa mtu mwingine wala Viongozi tuache kuingilia majukumu ya watendaji ambayo yako kisheria,"alisema Msofe.

Pia Mkuu huyo wa Wilaya amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kyerwa pamoja na madiwani kuhakikisha wanatumia wakaguzi wa ndani ili kupata dondoo mapema na kuzifanyia marekebisho haraka kabla ya ukaguzi wa nje kukuta hoja za kujibu.


No comments:

Post a Comment

Pages