Na Mashaka Mhando, Tanga
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, Alhamisi Novemba 16 anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi kwenye kongamano la uwekezaji lililolenga kutangaza fursa za uchumi .
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba ametoa kauli hiyo wakati Akizungumza na waandishi wa habari dhidi ya mpango huo ofisini kwake.
Kindamba amesema kongamano Hilo ambalo litakutanisha wawekezaji mbalimbali kutakuwa ni sehemu pekee ya kutoa picha halisi ya fursa ambazo zipo mkoa wa Tanga ambazo zinahitaji watu kuwekeza na hivyo kuchangia Kasi ya uchumi wa mkoa wa Tanga na na wa mtu Moja moja.
"Tukio hili ni kubwa na la kihistoria katika Mkoa Tanga kwasababu tukio laa aina hii liliwhi kufanyika miaka 10 iliyopita serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Haassan inaupiga mwingi kwa kumimina bilioni 429.1 na kuifanya bandari ya Tanga kuwa kati ya bandari kubwa lakini pia kuwa bandari yenye ubora, "alisisitiza Waziri Kindamba.
Katika mkutano huo na Wanahabari Kindamba akaeleza uwekezaji wa mabilioni ya shilingi ambayo tayari yameshawekezwa na serikali katika mkoa Tanga katika sekta mbalimbali.
Kongamano Hilo linalenga kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi kwenye mkoa wa Tanga yatakayosaidia kuwepo kwa ajira kwa wananchi wa Tanga na nje ya mkoa.
No comments:
Post a Comment