HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 12, 2023

Mbinu za kuondoa tatizo la watu kujiua Karagwe kuanza kutumika

 Na Lydia Lugakila, KARAGWE


Baraza la madiwani Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera limesema kutokana na wimbi kubwa la watu kujiua Wilayani humu unapaswa kuandaliwa utaratibu na mbinu kutoka kwa wataalamu kuanza kutoa ushauri nasaha kwa jamii ili kuondoa changamoto hiyo kwani inapunguza nguvu kazi ya Taifa.


Kauli hiyo imekuja baada ya Madiwani hao kutoa taarifa za kata na kata nyingi kuonesha wimbi kubwa la wananchi kujinyonga na kunywa sumu.


Akieleza hayo Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Wallesi Mashanda amesema inabidi kamati ya Ulinzi na usalama pamoja na idara ya ustawi wa jamii zifanye utafiti kujua nini chanzo cha Wananchi kujiua na utakapobaini ianze kutoa elimu kwa wananchi ili kuondoa changamoto hiyo.


Kupitia kikao hicho Mashanda amesema inabidi wananchi wajue umuhimu wao kuishi na kushiriki katika shughuli za maendeleo katika Taifa lao na sio kujikatisha uhai wa kuishi.

No comments:

Post a Comment

Pages