HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 30, 2023

Mbunge Byabato afanya makubwa Kagera

Na Lydia Lugakila, Kagera

Mhe. Stephen Byabato Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ametatua baadhi ya kero zilizodumu kwa muda mrefu kwa wananchi wanyonge zilizowasilisha kwake wakati wa kupokea kero kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Rwamishenye, baada ya kuhitimisha ziara yake kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo.

Mhe. Byabato  aliyeambatana na Kaimu Mkurugenzi pamoja na wataalamu kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, alionekana kuibua hisia za walio wengi huku wengine furaha ikawapelekea kutoa machozi kwa namna alivyoweza kushughulikia kero zao zilizodumu kwa muda mrefu na kuzipatia ufumbuzi yeye na wataaalam alioambatana nao.

Kero alizofanyia kazi ni pamoja na namna alivyoweza kulipa madeni Mawili ya Akina Mama wa kata ya Rwamishenye moja ya deni hilo ni lililohusu madai ya Askari wa Jeshi la Polisi Kituo cha Kati Bukoba, (Jina limehifadhiwa) aliyechukua Nguo zenye thamani ya Shilingi 162,000/= Dukani kwa Mama Mfanyabiashara Sharifa Leonard  na Kuahidi angemlipa lakini limekuwa deni la Muda mrefu licha ya mama huyo kuripoti Kero hiyo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa Kagera Bravius Chatanda.

Kufuatia hali hiyo Mhe. Byabato ameamua kulipa Deni na kwamba yeye atafuatilia madai hayo kwa ngazi husika Ili arejeshewe Pesa yake.

Deni jingine lililolipwa na Mhe. Byabato ni la Bi. Mwatatu Katakweba ambalo alikuwa akidai Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kutokana na Kushindwa kulipia Ankara ya Maji yaliyochotwa kwake kipindi cha Ujenzi wa Ofisi ya Mtendaji Kata Rwamishenye Miaka Minne iliyopita  ambalo ni jumla ya Shilingi 187,300/= ambazo nazo amesema atakwenda kuzidai kwa wahusika wazimrejeshee.

Katika hatua Nyingine Mhe Babyato ameshiriki kuchangia mchango wa Ofisi ya Mama Mlemavu anayejulikana kwa Jina la Vaileth Augustin Kiasi cha Shilingi Laki Moja ambaye yeye amewasilisha Ombi lake la Kupatiwa mtaji wa shilingi laki mbili na nusu kuendeleza ofisi yake, ambapo kiasi kingine kimechangwa na Wadau wengine kama kumpongeza Mama huyo kwa kujifungua Mtoto wa kike.

Aidha katika hatua nyingine Mhe. Byabato amekabidhi mkopo wa Shilingi laki moja kwa Kikundi cha akina Mama Rwamishenye walioamua kujiunga katika Shughuli ya Ufugaji Samaki ambao kwa kuanzia mahitaji yao yalikuwa ya vifaranga vya Samaki venye thamani ya shilingi laki nane, naye bila ajizi ametoa milioni moja kama Mkopo ikiwa ni Muendelezo wa Kutoa Mikopo ya KOPA KWA MBUNGE LIPA KWA MWENZAKO ambapo akina Mama hao watarejesha Ili wengine wakope bila riba.

Mbunge huyo ametoa shilingi laki tano kwa Wajasiliamali wanaofanya Shughuli zao jirani na Machinjio ya Rwamishenye, Ili kuboresha mazingira ya Biashara yao ya kuuza Utumbo na Viungo vingine vya Ndani ya Ng'ombe... Na Pesa hiyo haitarejeshwa kwani kaitoa Kuwaunga Mkono.

Hata hivyo amewapatia vijana wa UVCCM Kata Rwamishenye Mkopo Kutoka Mfuko wa KOPA KWA MBUNGE LIPA KWA MWENZAKO, ambapo Kiasi cha Shilingi Milioni moja kimekabidhiwa kwao Ili kuendeleza Mradi wao wa Ufugaji Samaki.

No comments:

Post a Comment

Pages