HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 30, 2023

CRDB yatoa msaada wa viti na meza katika Shule Mpya ya Sekondari ya Lingato

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo (katikati) akipokea sehemu ya msaada wa viti na meza kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Muhumiliza Buberwa (wa nne kushoto) vilivyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya shule mpya ya Lingato Sekondari iliyopo Kisarawe II. Wengine ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Pwani, Badru Idd (wa pili kushoto), Meneja wa CRDB Tawi la Kibada, (Isaya Lyimo), Meneja Mwandamizi Idara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Benki ya CRDB, Suzan Shuma (wa tatu kushoto), Kaimu Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Kigamboni, Emmanuel Mwakalinga (kulia), Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Lingato, Ashura Bihongo na Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kigamboni, Adellah Ntenjera, hafla hiyo ilifanyika Novemba 29, 2023 katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya. (Na Mpiga Picha Wetu).


 
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halim Bulembo (katikati) na Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Muhumiliza Buberwa, wakisaini nyaraka baada ya Benki ya CRDB kukabidhi msaada wa Viti na Meza kwa Shule Mpya ya Sekondari ya Lingato iliyopo Kisarawe II wilayani Kigamboni. 
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo (wa tano kushoto) akibadilishana hati na Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Muhumiliza Buberwa, baada ya makabidhiano ya viti na meza kutoka vilivyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya shule Mpya ya Lingato Sekondari iliyopo Kisarawe II wilayani humo. Wengine ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Pwani, Badru Idd (wa nne kushoto), Meneja wa CRDB Tawi la Kibada, Isaya Lyimo (kushoto), Meneja Mwandamizi Idara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Benki ya CRDB, Suzan Shuma (wa nne kulia) na Kulia ni Kaimu Afisa Elimu Wilaya ya Kigamboni, Emmanuel Mwakalinga (wa tatu kulia).

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo (katikati) na
Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Muhumiliza Buberwa, wakionyesha nyaraka baada ya makabidhiano ya Viti na Meza kwa ajili ya Shule Mpya ya Lingato Sekondari.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo (katikati), akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya Viti na Meza kwa ajili ya Shule Mpya ya Sekondari ya  Lingato iliyopo Kisarawe II. Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Pwani, Badru Idd na kulia ni Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Muhumiliza Buberwa.
   
Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Muhumiliza Buberwa, akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Viti na Meza kwa ajili ya Shule Mpya ya Sekondari ya Lingato. 

No comments:

Post a Comment

Pages