MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Albert Chalamila, amewataka wakazi wa
Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kusajili
watoto walio chini ya miaka mitano mara zoezi la kuwasajili watoto hao
litalapoanza rasmi jijini mapema mwezi ujao.
Akizungumza
jana kwenye semina ya mafunzo kwa waganga na viongozi kutoka wilaya
zote za Mkoa wa Dar es Salaam iliyoandaliwa na Wakala wa Usajili na
Udhamini (RITA) kama sehemu ya maandalizi kabla uzinduzi wa rasmi wa
zoezi hilo litakalohitimishwa kitaifa katika Mkoa wa Dar es Salaam. Bw.
Chalamila aliiambia semina hiyo kuwa vyeti hivyo vinatolewa bure na
kwamba Serikali tayari imebeba gharama zote.
"Nisisikie
mwananchi ametozwa pesa ili kupata cheti cha mtoto wake; vyombo vya
ulinzi na usalama vipo macho na vinafuatilia kwa karibu sana. Sote tuwe
makini na kila mmoja wetu atekeleze wajibu wake". alisema Bw.Chalamila.
Amewataka
wasajili wasaidizi kuhakikisha wanazingatia uadilifu, kujituma na
uzalendo na kusema hayo ni mambo ya msingi katika utekelezaji wa mpango
huo.
Ametaka viongozi wa dini na wazee maarufu washirikishwe katika utekelezaji wa zoezi hilo..
Afisa
Mtendaji Mkuu wa RITA, Bw. Frank Kanyusi, alisema kuwa chini ya mpongo
huo RITA inategemea watoto 248,298 wasajiliwe mkoani humo, kwani
watoto waliosajiliwa ni 624,755 au asilimia 60.3 ya watoto wanaostahili
kusajiliwa.
Alisema mpango huo umetekelezwa kwa mafanikio makubwa katika miaka 25 na kwamba Dar es Salaam ndiyo wa mwisho.
Mikoa
25 ya Tanzania Bara imeshapata huduma isipokuwa Mkoa wa Dar es Salaam
pekee. Hadi sasa zaidi ya watoto 8,886,778 wamesajiliwa na kupata vyeti
vya kuzaliwa ambavyo watavitumia kupata huduma nyingine za kijamii ikiwa
ni pamoja na kupata huduma ya matibabu kupitia mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya, elimu sambamba na ajira, alisema Bw. Kanyusi
Alisema
yamefanyika maboresho na mageuzi makubwa kupitia mpango huo ambapo
hivi sasa wamegatua majukumu ya usajili kwenda serikali za mitaa ambapo
watoto wanasajiliwa karibu na maeneo yao ya makazi; yaani katika vituo
vya tiba vinavyotoa huduma ya afya ya mama na mtoto na katika ofisi za
watendaji kata,alisema Bw. Kanyusi
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Bw Hosea
Mitala, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuupa uzito mpango huu, kupitia RITA.
Amewataka wakazi wa Dar es Salaam kuchangamkia hiyo fursa hiyo.
Tangu
mpango huo uzinduliwe na kutekelezwa katika mikoa 25 wazazi
wamewasajili watoto wao kwa bidii na kupata vyeti vya kuzaliwa bure na
kuifanya Tanzania isifike kimataifa katika suala hili.
No comments:
Post a Comment