Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Udalali ya Mahakama imeanza zoezi la kuwaondoka kwenye nyumba zake wapangaji wadaiwa sugu ambao ni Watumishi wa umma na viongozi wa Serikali.
Akizungumza na wanahabari jijini humo Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Dar es Salaam Arch. Bernard Mayemba amesema wameanza kuondoa wapangaji wa Nyumba za XNMC zilizopo Mbezi Beach.
Ameeleza kuwa zoezi hilo lilipaswa kuanza rasmi Nchi mzima Desemba 1, 2023, lakini kwa Mkoa wa Dar es Salaam wameamua kuanza leo kwamba hakuna cha kusubiri kwani notisi imeshaisha muda wake.
“Mkoa wa Dar es Salaam una jumla ya Nyumba 1200 za Watumishi wa umma waliopangisha, na kiasi kinachodaiwa kutoka kwa wapangaji ni shilingi bilioni 1.1,” amesema Arch. Mayemba.
Amesema kuwa zoezi hilo litafanyika kwa takribani wiki tatu na kuwa hawataangalia sura ya mtu na kwamba Fedha watakazopata kupitia madeni hayo yatawasaidia kukarabati Nyumba na miundombinu mingine ili kuhakikisha kunakuwa na Mazingira mazuri kwa wapangaji.
“Lakini pia zitasaidia kuboresha makazi mbalimbali na kuwapatia Watumishi wa umma makazi bora. TBA imekuwa ikitoa Makazi bora kwa Watumishi wa Umma.
Hata hiivyo ameeleza kuwa, pamoja na notisi kupita muda wake ni kwamba wapangaji watakaolipa madeni yao kabla ya kufikiwa na zoezi hilo hawataondolewa.
Amesema wakimaliza kuondoa wadaiwa sugu katika eneo hilo la XNMC Mbezi Beach watahamia Masaki, Mikocheni Oyesterbay, hivyo ameeleza kuwa wadaiwa wote wataguswa.
No comments:
Post a Comment