HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 29, 2023

Waziri PROF. Mkenda avitaka Vyuo Vikuu vya Afrika kushirikiana Uthibiti wa Ubora wa Elimu


 

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Vyuo vya Elimu ya Juu Barani Afrika ni vyema vikashirikiana katika kutoa mafunzo yenye ubora ili kuzalisha Wahitimu wenye sifa zinazokidhi viwango vya kimataifa.

Profesa Mkenda ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la kimataifa la wadhibiti ubora ya Elimu barani Afrika lililozileata pamoja nchi zaidi ya 22 kujadili mambo muhimu kuhusu Elimu ya juu, lililofunguliwa rasmi leo Novemba 28,2023 Jijini Dar es Salaam.

Amesema idadi ya Vyuo Vikuu na wanafunzi wanaosoma Elimu ya juu inazidi kuongezeka, hivyo ni vyema suala la ubora wa Elimu likazingatiwa ili kuwa na Wahitimu wenye sifa.

""Washiriki watumie nafasi hii kujadili namna ya kuhakikisha ubora wa vyuo vikuu unakuwa vilevile. Changamoto tulizonazo ni kuongeza wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja na ubora sababu wakiwa wengi watashindwa kufanya utafiti," alisema Prof. Mkenda.

Amesema kuwa Ili elimu ya juu iwe bira kunatakiwa kuwa na wakufunzi wenye sifa zinwzokidhi viwango vya kimataifa na kwamba Wanafunzi wanatakiwa kupata ufaulu mzuri ili waweze kumudu ushindani katika soko la ajira.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini –TCU , Prof Charles Kihampa amesema kongamano hilo litasaidia kuweka mikakati ya pamoja ya kuendelea kutoa Elimu Bora Kwa wanafunzi wa Elimu ya juu.

"Kongamano hili lina manufaa kwa kuwa elimu ya juu sio ya nchini kwako tu, Kuna umuhimu sa kushirikiana katika ubora ili mhitimu aweze kuajirika ndani na nje ya nchi," alisema Prof. Kihampa.

No comments:

Post a Comment

Pages