HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 08, 2023

GAMONDI AISUKA UPYA SAFU YA ULINZI

NA MWANDISHI WETU


Mkuu wa Benchi la Ufundi wa Yanga SC Miguel Gamondi, ameweka wazi kuwa watafanyia kazi makosa katika mechi za kimataifa upande wa ulinzi ili kutoruhusu mabao mengi ya kufungwa.



Hayo yanajiri mara baada ya kuruhusu mabao manne katika mechi mbili ambazo wameshuka dimbani mpaka sasa katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAF CL

Katika mabao hayo manne Yanga imeruhusu ugenini dhidi ya CR Beloizdad mabao 3-0 huku wakiruhusu bao moja kwenye sare ya bao 1-1 dhidi ya Al Ahly.


Gamondi amesema kuwa makosa waliyofanya kwenye mechi za kimataifa ni sehemu ya mchezo jambo ambalo linafanyiwa kazi katika uwanja wa mazoezi.


“Utaona kwamba mabao ambayo tulifungwa ilitokana na namna ya kuzuia makosa ambayo tulifanya. Hapo ni muhimu kwetu kuangalia namna ya kurejea katika ubora na sehemu ya mazoezi tunafanyia kazi hayo.


Kikubwa ni kuona kwamba hatufanya makosa mengi kwenye eneo letu la hatari kwani wapinzani nao wanatafuta matokeo, hivyo hilo tunalifanyia kazi kwa ajili ya kuwa imara kwa mechi zijazo.”


Safu ya ulinzi ya Yanga inayotarajiwa kuvaana na Medeama ya Ghana Desemba 8 inaongozwa na Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Bacca.
Mwisho

No comments:

Post a Comment

Pages