Mmoja
wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii katika Kata ya Gendabi Wilaya ya
Hanang Mkoani Manyara akitoa elimu namna ya kutumia dawa ya kutibu maji
ili kuweka tahadhari ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwemo
Kipindupindu.
Wawakilishi kutoka Wizara ya Afya, Wahudumu wa Afya ngazi ya
Jamii kata ya Gendabi Wilayani Hanang wakiwa pamoja na moja ya familia
iliyopatiwa elimu namna ya kutumia dawa ya kutibu maji katika Kujikinga
na Magonjwa ya Mlipuko.
Na Elimu ya Afya kwa Umma
Wananchi kutoka katika kata za Gendabi na Katesh Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara wameipongeza Serikali kwa kuweka jitihada za pamoja katika kuhakikisha wanapata maji safi na salama baada ya kuanza kutoa dawa ya kutibu maji bure nyumba kwa nyumba.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti nyumbani kwao mara baada ya kutembelewa na Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kutoa elimu namna ya utumiaji sahihi wa dawa za kutibu maji, baadhi ya wananchi hao akiwemo Innocent Ally wamesema dawa hiyo itawasaidia kutibu maji katika kuondoa vimelea vya magonjwa.

“Tunaishukuru serikali kwa dawa mliotuletea hii dawa ni tiba inayofanya maji kuwa safi na salama naishauri jamii hii ya Gendabi tutumie dawa hii inayotibu maji,namshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alisitisha ziara yake kuja hapa Hanang, Taifa limehamia Hanang Mungu azidi kuwainua katika kazi zenu” amesema Innocent.
Kwa upande wao Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii akiwemo Selestina Salwatt Mratibu wa Afya Ngazi ya Jamii Wilaya ya Hanang wamesema wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na uelewa jinsi ya kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo utumiaji sahihi wa dawa ya kutibu maji.
“Tunatoa elimu kwa jamii namna nzuri ya kutumia dawa ya kutibu maji katika kujikinga na magonjwa ya mlipuko na lita 20 ya maji unaweka vidonge viwili na lita 10 ya maji unaweka kidonge kimoja “ wamesema.
No comments:
Post a Comment