Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linawatafuta watuhumiwa wa kosa la kuharibu mali katika kijiji cha Halungu-Mbozi.
Disemba 18, 2013 huko Kata ya Halungu wilaya ya Mbozi mkoani
Songwe shamba la mahindi lenye ukubwa wa heka 11 lililolimwa na watu 04
walilokodi kwa Edina Mgala, shamba hilo alilikodisha kwa kuligawa kwa
watu hao ambao ni Mailo Msangawale (35) alikodishiwa heka 07, Emi
Magwaza (48) alikodishiwa heka 1.5, Salome Nkota (50) alikodishiwa heka 1.5, na Jeremia Ngoya (42) alikodishiwa heka 1 wote ni wakulima na ni wakazi wa Halungu.
Heka hizo zimeharibiwa baada ya kupuliziwa dawa ya kuulia magugu aina ya Rounup na mtu/watu wasiofahamika.
Uchunguzi
wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa ardhi
unaohusisha familia mbili kati ya watoto wa mke mkubwa na mke mdogo wa
marehemu Focus Makonongo.
Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe
kwakushirikiana na maafisa kilimo wilaya ya Mbozi linafanya tathimini
ili kuweza kujua thamani halisi ya mali iliyoalibiwa pamoja na kemikali
iliyotumika kufanya uharibifu huo.
Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe
linatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za mtu au watu ambao wamehusika
katika tukio hilo ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za
kisheria.
Aidha Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe linatoa rai kwa
wananchi kutokujichulia sheria mkononi badala yake kutatua migogoro kwa
kukaa vikao na kusuluhisha kwa amani.
No comments:
Post a Comment