WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma, akizungumza katika Maonesho ya mavazi ya wiki ya ya Mafunzo ya Amali yanaliofanyika katika viwanja vya Mapinduzi Square Michenzani Mjini Unguja.
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma ameitaka jamii kuacha tabia ya kuiga tamaduni za kigeni ambazo haziendani na mila, silka na utamaduni wa kizanzibari ikiwemo suala la mavazi na malezi.
Mhe.
Pembe ameyasema hayo katika Maonesho ya mavazi ya wiki ya ya Mafunzo ya
Amali yanaliofanyika katika viwanja vya Mapinduzi Square Michenzani
Mjini Unguja, amesema mavazi ya staha ni moja ya Utamaduni wa
wazanzibari hivyo ni vyema kuendelezwa na kuacha kuiga mavazi ambayo
hayana staha.
Amefahamisha
kwamba mavazi ya staha na malezi bora ni njia moja wapo ya kuzuia
vitendo vya ukatili na dhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto ambavyo
vinajitokeza kila mara ndani ya jamii.
“suala
la kuiga tamaduni zisizo za kizanzibari ambazo baadhi yake ndio sababu
kubwa ya mporomoko wa maadili ya nchi na kusababisha vitendo vya
udhalilishaji kuongezeka kila siku ni vyema kuachana nazo na badala yake
kuendeleza mila, silka na Utamaduni wa Zanzibar” Alisema Waziri huyo.
Mhe.
Riziki katika hafla hiyo ameomba Mamlaka ya Mafunzo ya Amali pamoja na
Vyuo vyengine kuanzisha madawati ya kijinsia katika vyuo vyao ili iwe
rahisi kwa wanafunzi wanapopata tatizo au kuona viashiria vya
Udhalilishaji waweze kutoa taarifa kwa haraka kuhusu kupinga vitendo vya
udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto.
Aidha
ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao katika vyuo
hivyo vya Mafunzo ya Amali ili kupata taaluma na ujuzi utakaowasaidia
vijana kupata ajira na kujiongezea kipata hali ambayo itawasaidia
kuinuka kiuchumi.
Mwisho
amewaomba Wanafunzi waliomaliza mitihani yao ya Kidato cha nne na hata
wale ambao wapo majumbani kujiunga na vituo/vyuo vya mafunzo ya amali
kwani ni miongoni mwa fursa za kuweza kujiajiri na kuondokana na
umasikini.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt.Bakari
Ali Silima amesema maonesho ya mavazi ni moja wapo ya kuonesha kazi
zinazofanywa na vyuo hivyo, hivyo ni vyema jamii kuangalia ili kujifunza
na kuona ni sehemu sahihi ya kuwapeleka watoto wao kupata ujuzi.
Akizungumza
kwa niaba ya washiriki wa mavazi hayo Fatma Ali amesema vazi la staha
linasaidia kumpa mtu ujasiri wa kukutana na watu mbali mbali katika
harakati za maisha kwani mavazi ni mawasiliano katika jamii husika.
No comments:
Post a Comment