HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 29, 2023

M/KITI KAWAIDA: MATEMBEZI YA MIAKA 60 YA MAPINDUZI YAMEIBUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA PEMBA

NA IS-HAKA OMAR, PEMBA

 

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Taifa Mohamed Ali Kawaida,amesema Umoja huo unaimarisha mazingira bora ya makaazi ya watendaji wake yaendane na hadhi ya taasisi hiyo.

 

Hayo ameyasema wakati akizungumza na maelfu ya vijana wa UVCCM wanaofanya Matembezi ya kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar  mara baada ya kushiriki ujenzi wa Taifa katika mradi wa ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Mkoa wa Kusini Pemba.

 

Alisema mradi huo unaendana na dhamira ya UVCCM kwa kuhakikisha kila mtendaji anafanya kazi zake akiwa katika makaazi bora.

 

"Tukio hili la ushiriki wa ujenzi wa Taifa limeshirikisha Vijana kutoka Mikoa yote ya Tanzania, ambapo imeacha alama kwa kuanzisha mradi wenye manufaa makubwa katika maisha ya kila siku ya Watendaji wetu",alisema Kawaida.

 

Katika maelezo yake Kawaida, alisema UVCCM inaendelea kubuni na kuibua fursa za kimaendeleo ili vijana wote wanufaike.

 

Alieleza kuwa miaka 60 ya Mapinduzi ni chachu ya kuendeleza mambo mema yaliyotekelezwa na waasisi wa Mapinduzi hayo yaweze kutekelezwa kwa kufuata mahitaji ya Vijana wa sasa katika nyanja za kiuchumi,kisiasa na kimaendeleo.

 

Pamoja na hayo aliwapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi kwa utekelezaji kwa ufanisi Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 Mijini na Vijijinj.

 

Matembezi hayo yanayowashirikisha Vijana 1000 kutoka Mikoa yote ya Tanzania yamezinduliwa Disemba 28,mwaka 2023 katika Mkoa wa Kusini na leo Disemba 29,mwaka huu yanaendelea Mkoa wa Kaskazini Pemba.

 

CAPTIONS

Picha no.001-MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mohamed Ali Kawaida,akishiriki ujenzi wa Taifa katika mradi wa Ujenzi wa Nyumba ya Katibu wa UVCCM Mkoa wa Kusini Pemba,katika Matembezi ya kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi.

Picha no.003-Vijana wa kikundi Maalum cha kubeba picha za Waasisi wa Mapinduzi na Viongozi wa sasa waliopo madarakani ambao ni aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Abeid Aman Karume,aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl.Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi.

Picha no.005-BAADHI ya Vijana wa UVCCM wakishiriki kazi mballimbali za ujenzi wa Taifa katika mradi wa Nyumba ya Katibu wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Kusini Unguja.

Picha no.006,007-BAADHI ya Vijana wakitembea kwa ukakamavu katika matembezi hayo kutoka Mkoa wa Kusini Pemba kuelekea Kaskazini Pemba.

Picha no.004-VIONGOZI wa Matembezi hayo wakitembea kwa ukakamavu kutoka Mkoa wa Kusini Pemba kwenda Kaskazini Pemba.

 

No comments:

Post a Comment

Pages