Na John Marwa
UONGOZI wa Simba. SC upo katika hatua za mwisho ya mazungumzo na winga wa kulia kutoka klabu ya Comerciantes FC ya Colombia, Mauricio Cortes kwa makubaliano ya kusaini mkataba wa miaka miwili.
Katika usajili wa dirisha dogo, Simba imepanga kusajili wachezaji wanne hadi watano ikiwemo nafasi ya ushambuliaji, kiungo mshambuliaji, winga na mlizni wa kushoto.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari ndani ya Simba, viongozi wanamawasiliano ya moja kwa moja na mchezaji na wakala wake na makubaliano yamekamilika.
"Baadhi ya klabu zilifanya mawasiliano na mawakala wa nyota huyo, lakini Simba walikuwa na ofa iliyoboreshwa, skauti mkuu na kocha Benchikha wote wamekamilisha dili hilo.
Simba itamtangaza nyota huyo wakati wowote na kuanzia Januri 2, mwakani anatarajia kutua nchini kujiunga na kikosi cha wekundu wa Msimbazi," kimeeleza chanzo chetu cha habari ndani ya Simba.
Mtendaji Mkuu wa Simba, Iman Kajula hivi karibu alisema wametenga fungu la kutosha kwa ajili ya kufanya usajili wa nguvu kwenye dirisha dogo ambalo lilifunguliwa wiki iliyopita.
Alisema wamemruhusu Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha sababu ndiye anayehusika moja kwa moja na usajili, tayari kocha huyo amefanya mapendekezo yamewafikia kwenye meza yao na tayari fungu la usajili limeshatengwa na tayari kufanyia kazi.
“Kocha ametuletea mapendekezo yake ametuambia mapungufu yaliyopo kwenye kikosi na aina na idadi ya wachezaji anaohitaji kusajili kwenye dirisha dogo na uongozi umemkubalia na kumtengea fungu la kutosha kwa ajili ya kupata saini za hao wachezaji,” alisema Kajula.
Alisema mikakati ya uongozi ni kuhakikisha wanamtimizia Benchikha mahitaji yake muhimu ili kuiboresha timu hiyo iweze kurudisha heshima iliyopotea katika michuano ya ndani na kufika Nusu Fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Aliongeza kuwa kamati yao ya usajili ipo karibu na Benchi la Ufundi kuhakikisha wanawapata wachezaji ambao kocha anawahitaji ili kukiimarisha kikosi chake ambacho kwa sasa kipo nafasi ya tatu kwenye Msimamo wa Ligi Kuu na kinapambana kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
December 30, 2023
Home
Unlabelled
MNYAMA SIMBA ATUA KWA MCOLOMBIA, MAMBO NI MOTO
MNYAMA SIMBA ATUA KWA MCOLOMBIA, MAMBO NI MOTO
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment