'SUPER STAR' wa kimataifa kutoka India, ambaye kesho Jumamosi Desemba 30 ataongoza mbio za urafiki kati ya India na Tanzania 'India-Tanzania Friendship Run', ameahidi kutoka sapoti kwa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), katika maeneo mbalimbali.
Milind, alibainisha hayo leo Ijumaa Desemba 29 wakati alipoendesha warsha kwa viongozi na wadau wa michezo ya Riadha, Kuogelea na sekta ya Filamu, kwenye kituo cha Utamaduni cha Watu wa India, Masaki jijini Dar es Salaam.
Mbali na hilo, pia alitoa ushauri namna ya kubuni na kuandaa matukio ya Riadha na kuyafanya yawe makubwa na kuvutia jamii kwa wigo mpana.
Pia kwa pamoja, Milind na viongozi wa RT, walijadili ya kuboresha zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na India katika nyanja ya mashindano ikiwemo uhusiano wa karibu uliokuwepo zamani na uongozi wa Pune Marathon, miundombinu, mabadilishano ya mafunzo, wanariadha wa India kupata fursa ya kushiriki NBC Dodoma Marathon na wanariadha wa Tanzania kushiriki mashindano mbalimbali India.
Ratiba ya kesho inatarajiwa kuanza saa 11 alfajiri Jumamosi kwa mbio za Kilomita 5 na 10, kisha Milind Soman akiungana na wanariadha wengine wa Tanzania watakuwa mbio ndefu Dar- Bagamoyo Kilomita 60 ambako watapumzika na Jumapili watarejea tena viwanja vya Farasi.
No comments:
Post a Comment