Arusha, Tanzania
Washindi
120 wa kampeni ya Benki ya NMB ya mastabata- halipoi wamejinyakulia
jumla ya zaidi ya shilingi milioni 24 kama zawadi katika droo yake ya
pili ya mwisho wa mwezi huu wa disemba ya kampeni hiyo inayolenga
kuhamasisha matumizi ya kadi na kulipa kwa kuskani QR katika kufanya
malipo.
NMB imegawa
zawadi hizo disemba 29 kwenye droo maalum iliyochezeshwa jijini Arusha,
ambapo pia washindi watatu wamefanikiwa kushinda safari ya Kendwa Rocks
na wenza wao huko Zanzibar watakaogharamiwa usafiri, malazi na chakula
pia posho ya shilingi 200,000.
Droo
hiyo ilitoa washindi 100 wa kila wiki waliojishindia kila mmoja
shilingi 100,000 na wateja 17 wa mwezi waliojishindia kila mmoja
shilingi 500,000 taslim.
Akizungumzia
droo hiyo, wakati wa ugawaji wa zawadi, Meneja Mwandamizi wa NMB Idara
ya Biashara ya Kadi, Manfredy Kayala, amesema washindi hao 120 ni wa mwezi
huu ambapo wamegawiwa jumla ya shilingi 24.5 ikiwemo milioni 10 za
washindi 100 wa kila wiki ambapo kila mmoja alijishindia shilingi
100,00.
"Mbali na hao,
washindi 17 wa mwezi wamejishindia shilingi 500,000 kila mmoja, huku
washindi watatu wakipata safari ya kugharamiwa kwenda Zanzibar na wenza
wao na watapewa posho ya 200,000 " alisema Kayala.
Kayala
alisema kuwa zawadi hizo ni sehemu ya zawadi ya shilingi milioni 350
walizotenga kutoa kama zawadi zikiwa ni pesa taslimu pamoja na safari za
kwenda kupumzika katika visiwa vya Zanzibar na nchini Afrika Kusini.
"Kwa
kampeni hii ya awamu ya tano, kuna zaidi ya washindi 1200 wa kila wiki
wanaopata 100,000/- katika kampeni zinazoendelea pamoja na washindi 240
wa papo hapo ambao wanapata 50,000/- wanapofungua akaunti au kujibu
maswali kadhaa. Hiyo ni pamoja na washindi wa kila mwezi ambao kila
mmoja atapata 500,000/" alisema.
Alisema
kampeni hiyo inalenga kuhamasisha matumizi yasiyotumia fedha taslim na
badala yake watumie kadi, kuskani QR au malipo ya kiktandao ambayo
itapunguza kiwango cha uhalifu unaohusisha watu kuibiwa fedha zao kama
ilivyokuwa zamani lakini pia kukuza uchumi.
Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Praygod
Godwin alieleza kuwa promosheni hiyo maalum inatekelezwa na benki hiyo
kwa kushirikiana na kitengo Mastercard.
Alisema
Benki hiyo yenye matawi zaidi ya 43 Kanda ya kaskazini,
itaendeleabkujanna promosheni mbalimbali ili kuendelea kuwanufaisha
wateja wanaotunia huduma za Benki hiyo.
“Ukiwa na Kadi ya NMB mtu anaweza kufanya miamala wakati wowote na mahali popote ambapo kuna Pointi za Mauzo (POS) ".
Mmoja
wa wateja walioshinda droo hiyo, mfanyabiashara Jackline Matowo,
alisema alienda benki kuweka pesa kwa ajili ya biashara yake lakini
akabahatika kucheza droo ya papo hapo na kushinda shilingi 50,000/-
katika kampeni inayoendelea.
"NMB
wamefanya kampeni nzuri haswa ambayo inahamasisha wateja kuendelea
kutumia huduma za kifedha kidigitali kwa kutambua zawadi hizi lakini
inaleta usalama wa fedha zetu na zaidi inasaidia nchi kujua maendeleo
yake kiuchumi" alisema.
No comments:
Post a Comment