HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 11, 2023

PBPA: Ruzuku ya Serikali yapunguza makali ya bei ya Mafuta

Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement Agency - PBPA), Erasto Simon, akitoa walisho lake kwenye kikao kazi baina ya Wakala na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) na kufanyika jijini Dar es Salaam, leo Disemba 11, 2023.

Afisa Mwandamizi wa Habari na Mawasiliano kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) Sabato Kosuri, akifafanua jambo wakati akifungua Kikao kazi baina PBPA na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na OTR na kufanyika Jijini Dar es Salaam Disemba 11, 2023. Kushoto ni Mkaguzi Petroli PBPA, Bruno Tarimo na katikati ni Mkaguzi wa Ndani, Juma Hamidu. 

 

Baadhi ya wahariri wakiwa katika mkutano huo.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Yassin Sadiki, akitoa neno la shukrani baada ya wakati wa Kikao Kazi baina ya Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) na Wahariri wa Habari kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR).
 

 

Na Mwandishi Wetu

 

Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement Agency - PBPA) imesema kuwa katika kipindi cha  miezi sita kuanzia Julai 2022 hadi Disemba 2022 Serikali imetoa ruzuku ili kupunguza bei ya mafuta kwa wananchi hatua ambayo ilifanyika baada ya athari ya bei ya mafuta kupanda sana katika soko la dunia kutokana na vita baina ya Urusi na Ukraine.

 

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement Agency - PBPA) Erasto Simon, kwenye kikao kazi baina ya Wakala na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) jijini Dar es Salaam, leo Disemba 11, 2023.

 

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za makusudi kupunguza makali ya bei ya mafuta nchini ikiwemo kutoa ruzuku kwenye gharama ya mafuta, bei za nishati hiyo zinapopaa kutokana na changamoto mbalimbali za kidunia.

 

Simon alizitaja hatua nyingine zilizochukuliwa na Serikali ni pamoja na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maghala ya kuhifadhia mafuta ili kuhakikisha taratibu za uendeshaji wa maghala hayo zinazingatiwa.  


Aidha Simon alisema kuwa pamoja na Serikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha nishati ya mafuta inapatikana kwa wakati, ikiwa bora na bei stahmilivu, alieleza malengo na mafanikio yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa na PBPA.

 

Akizungumzia uwezo wa maghala ya kuhifadhi mafuta Mkurugenzi huyo alisema kuwa Tanzania ina  maghala 22 yenye uwezo wa kupokea mafuta kutoka kwenye meli katika Bahari ya Hindi ambayo yana uwezo wa kupokea lita bilioni 1.31 kwa aina nne za mafuta ya petroli (dizeli, petroli, mafuta ya ndege & mafuta ya taa.

 

Katika Mgawanyo wa maghala hayo kwa upande wa Kurasini jijini Dar es Salaam ina jumla ya maghala 11 yenye uwezo wa kupokea takriban jumla ya lita milioni 570 huku Kigamboni ikiwa na maghala nane yenye uwezo wa kupokea takriban lita milioni 522 huku Mtwara ikiwa maghala mawili yenye uwezo wa kupokea takriban lita milioni 35 na Tanga ikiwa  na ghala moja lenye uwezo wa kupokea lita milioni 182.

No comments:

Post a Comment

Pages