Na Elimu ya Afya kwa Umma
Kutokana na Serikali kuweka msukumo wa kutoa elimu ya afya katika kujikinga na magonjwa ya mlipuko wilayani Hanang Mkoani Manyara ikiwemo ugawaji wa vipeperushi vya uelimishaji pamoja elimu ya matumizi sahihi ya dawa ya kutibu maji , baadhi ya wananchi wilayani humo wameipongeza serikali kwa kuweka kipaumbele uelimishaji.
Wakizungumza katika vijiji vinavyozunguka mlima wa Hanang baadhi ya wananchi hao akiwemo mwenyekiti wa Kijiji cha Gendabi wamesema kuwa serikali imefanya jambo jema kutoa elimu ya afya kuhusu kujikinga na magonjwa ya mlipuko pamoja na ugawaji wa vipeperushi kwani itasaidia kuchukua hatua stahiki za kujikinga na magonjwa ya mlipuko hasa katika kipindi hiki cha masika.
“Hili janga na mafuriko na tope kutokana mlimani limepita, ila kutokana na vyanzo vya maji kuchangamana hasa kwa miundombinu na maji ya mafuriko kunaweza kutokea jambo jingine kama vile magonjwa ya kuhara na kutapika,lakini serikali yetu imeona mbali tunashukuru serikali imetujali I kwa kuwatumia hawa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii tunapewa dawa ya kutibu maji pamoja na kupewa vipeperushi bure”amesema mmoja wa wananchi.
No comments:
Post a Comment