HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 13, 2023

SIMBA SC WAENDELEA NA SHABIKI BINGWA KIBABE


NA JOHN MARWA 


Klabu ya Simba imeendelea kuwashukuru mashabiki wake kwa kuunga mkono timu yao wakati huu ambao inaendelea  kuimarika, leo hii uongozi wa Simba umekuja na kitu cha zaida kurudi kwa mashabiki wao. 



Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo Imani Kajula ambapo amesema, moja ya wajibu mkubwa wa shabiki wa Simba ni kuisaidia timu yao kwa kununua bidhaa za klabu hiyo.

“Unaponunua bidhaa ya klabu unaisaidia klabu kujijenga kwenye mifumo yake ya kifedha. Ni wazi kwamba uendeshaji wa vilabu ni gharama sana. Ili tuwe na benchi bora, wachezaji wazuri, walipwe mishahara, wakae vizuri, walipwe posho, wasafiri. Ndio maana katika klabu yenu bajeti kwa mwaka ni Tsh. 24 Bilioni.”

“Mwaka huu tulianza na Shabiki Bingwa ambapo mashabiki wanashinda fedha taslimu, safari, tiketi za mechi na wakati hii kuelekea sherehe za mwisho wa mwaka tumekuja na MFALME SHANGWE. Mfalme ni Simba, shangwe ni kuelekea mwisho wa mwaka. Tumekuja na shindano ambalo lina jumla ya zawadi zisizopungua Tsh. 500 milioni na kushinda zawadi ya tiketi za mechi.” Amesema CEO Imani Kajula.
“Simba inaamini kwenye mashabiki wake kuwa na faida, kama atakuwa ni shabiki ambaye anaeleza mambo ambayo anataka lakini hashiriki kuisaidia timu basi ni ushabiki usio na faida. Kwa mashabiki wa faida basi MFALME SHANGWE ni jambo la kushiriki.”

“Eneo moja wapo ambalo litafaidika na mapato ambayo yatapatikana kupitia MFALME SHANGWE ni eneo la timu ya vijana. Mwaka huu tulitafuta vijana bora sana nchini. Mfano tuna vijana 15 katika timu ya vijana ya Zanzibar ambayo ilishinda ubingwa wa CECAFA. MFALME SHANGWE inaunganishwa na maendeleo ya timu kwa ushabiki wenye faida.”

“Tunawakaribisha Wanasimba na mashabiki wa soka Tanzania kushiriki MFALME BINGWA. Tunaamini tutaendelea kujitahidi ili Simba iwe sehemu ya furaha yenu kuelekea mwisho wa mwaka huu.” Imani Kajula
Mwisho


No comments:

Post a Comment

Pages