NA VICTOR MASANGU, MKURANGA
Mamlaka
ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani imeamua kujikita katika
kuboresha sekta ya afya kwa kutoa msaada wa vifaa mbali mbali katika
Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga ikiwemo kitanda maalumu kwa ajili ya
kujifungulia wakinama pamoja na magodoro 20.
Hayo
yamebainishwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Pwani Masawa Masatu wakati wa
halfa fupi ya kukabidhi msaada huo ikiwa ni ni mwendelezo ya wiki ya
kutoa shukrani kwa mlipa kodi wake pamoja na kufanya matendo ya huruma.
Meneja
huyo ambaye katika halfa hiyo pia aliambatana na maafisa wengine wa TRA
ikiwa sambamba na viongozi wa serikali ambao waliweza kufika katika
hospitali hiyo kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali katika
kuboresha huduma ya afya.
Kadhalika
Meneja Masawa alibainisha kuwa pia wamesherekea siku hiyo kwa kutoa pia
mashuka 50,Magodoro 20 taupo za kike,pamoja na mahitaji mengine mbali
mbali ya msingi vyote vikiwa na zaidi ya milioni tano.
"TRA
Mkoa wa Pwanin tupo katika maadhimisho ya wiki ya shukurani Kwa walipa
kodi wetu na leo tumepata fursa ya kutembelea katika hospitali ya
Wilaya ya Mkuranga na tumekabidhi misaada mbali mbali ambayo pia
itasaidia kwa wagonjwa hasa kwa wakinamama,"alibainisha Masawa.
Pia
aisema kwamba wana tambua kwamba sekta ya afya ni muhimu sana hivyo
wana imani misaada hiyo ambayo wameitoa itaweza kupunguza baadhi ya
changamoto ambazo zilikuwa zikiikabili hospitali hiyo ya Wilaya ya
Mkuranga kwani wagonjwa wataweza kutibiwa katika mazingira rafiki.
Kwa
upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Angelus Mtewa,alisema
kwamba wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upungufu wa vitanda hasa
katika wodi ya mama na mtoto.
Alisema
kuwa wakati mwingine kutokana na uhaba huo inawalazimu baadhi ya
wakinamama muda mwingine kulala wagonjwa watatu katika kitanda kimoja
hali ambayo inasababisha msongamano.
Mganga
huyo hakusita kuishukuru TRA Mkoa wa Pwani kwa kutumia wiki ya mlipa
kodi kwenda kutoa msaada wa vifaa mbali mbali ambavyo vitakuwa ni
chachu katika kuongeza ufanisi ya kutoa huduma ya matibabu kwa wananchi.
Alisema,
jengo la mama na mtoto lilipo katika hosptali hiyo linauwezo wa
kuhudumia wanawake 70 Kwa mwezi lakini huudumia wanawake zaidi ya 500
Kwa mwenzi Hali ambayo imesababisha upungufu wa vitanda na baadhi ya
vifaa tiba.
"Jengo letu
Lina uwezo wa kuhudumia wanawake 70 tu Kwa mwezi lakini tunahudumia
wanawake zaidi ya 500 tofauti na mahitaji hivyo wengi wanalala watatu
katika kitanda kimoja na unakuta mama amejifungua Kwa upasuaji"alisema
Mtewa
Aidha alisema
mahitaji ya vitanda vya kuwalaza wanawake baada ya kujifungua ni zaidi
ya 50 na kwamba vilivyopo ni vitanda 18 pekee huku vitanda vya
kujifungulia vikiwa nane na mahitaji yakiwa vitanda 20.
"Changamoto
nyingine ni jengo letu ni dogo halitoshelezi mahitaji, wanawake wengine
wanalala chini na tena wamefanyiwa upasuaji, hivyo tunaishikuru TRA Kwa
kutupatia msaada Ila bado tunahitaji misaada zaidi kutoka kwa wadau
wengine,"alisema
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga, Arafa Halifa,aliongeza
kwamba msaada ambao wamepatiwa na TRA Mkoa wa Pwani utakuwa ni mkombozi
katika kusaidia kupunguza changamoto ya wakinama kujifungua hasa katika
wodi ya wazazi.
No comments:
Post a Comment