NA VICTOR MASANGU, MKATA
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA)
Kiula kingu amefika katika kata ya Mkata iliyopo halmashauri ya Tanga
Vijijini kutekeleza kwa vitendo agizo lililotolewa na Waziri wa Maji
Juma Aweso la kutaka kuimaliza kero na changamoto ya maji ambayo
inawakumba wakazi wa eneo hilo.
Aweso alitoa agizo hilo wakati
wa ziara ya kikazi ya Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Taifa, Paul Makonda ambapo msafara wake uliposimama
katika eneo hilo la Msata ukitokea Mkoani Pwani na kuagiza huduma ya
maji safi na salama iwafikie wananchi hao.
Akizungumza
mara baada ya kuwasili katika eneo hilo ikiwa ni katika kutekeleza
maagizo hayo ya Waziri Kaimu mtendaji huyo wa Dawasa Kiula alisema
kwamba kwa sasa wakazi wa eneo hilo la Msata wanapata maji ambayo sio
toshelevu kutoka na kuwepo kwa ongezeko kubwa la idadi ya wananchi.
"Kimsingi
tumefika katika eneo hili la Msata mashariki na hii ni hii tunatekeleza
wito na maagizo ambayo yametolewa na Waziri wa maji Juma aweso kwa
hivyo tumefika ili kuitatua changamoto hii ya maji,"alisema Kingu.
Kingu
alibainisha kwamba katika eneo hilo sio kwamba halina huduma ya maji
safi na salama isipokuwa maji yaliyipo kwa sasa hayawezi kutosheleza
kutoka na kuwa na ongezeko kubwa la wakazi ambao wanafikia zaodi ya elfu
90.
Aidha aliongeza
kuwa mipango ambayo inafanyika kwa sasa na Dawasa ni kufanya jitihada
za haraka katika kupeleka huduma ya maji kupitia chanzo cha maji
kilichopo kutoka tenki la maji lililopo kijiji cha Manga.
Pia
alibainisha kuwa sambamba na kuongeza wingi wa maji pia Mamlaka
itahakikidha itaboresha miundombinu yote ya maji ambayo ipo katika
kata ya Mkata ili iweze kuhudumia wananchi kwa urahisi.
"Ukiangalia
eneo hili la mkata wakazi wanazidi kuongezeka zaidi ukilinganisha na
siku za nyuma hivyo ni lazima tuweke mipango ya kuboresha miundombinu ya
maji na kuvuta maji kutoka maeneo ya jirani na hii itasaidia sana kwa
wananchi kupata maji ya uhakika.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Mkata Mashariki , Zamini Kafuluma
ameupongeza uongozi wa DAWASA kwa kufika katika eneo hilo kwa lengo la
kujionea na kutekeleza maagizo ambayo yametolewa na Waziri wa Maji
pamoja na Katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama cha mapinduzi (CCM)
Taifa.
Mwenyekiti huyo
aliongeza kitendo walichokifanya Dawasa ni kutekeleza Ilani ya chama kwa
vitendo kwa lengo la kuhakikisha wanasogeza huduma ya upatikanaji wa
maji safi na salama kwa wananchi.
Siku
chache zilizopita Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha Mapinduzi
,(CCM) Taifa Paul Makonda alipokuwa katika ziara yake ya kikazi akiwa na
Waziri wa Maji Juma Aweso walitoa maagizo kwa uongozi wa Dawasa kufika
katika eneo la Msata mashariki ili kutatua ya maji kwa wananchi jambo
ambalo limeanza kutekelezwa kwa vitendo na Dawasa.
No comments:
Post a Comment