Kwa kawaida Povu la maji katika maeneo ya mto husababishwa na kuwepo kwa kuoza kwa viumbe hai (Organic matters), kama vile mimea au mwani, ndani ya maji.
Wakati nyenzo hizi za kikaboni zinavunjika (Kuoza), hutoa “compounds” inayoitwa “surfactants” ambayo hupunguza mvutano wa maji.
Upungufu huu wa mvutano wa maji husababisha kuundwa kwa bubbles na povu. Hali hii hutokea zaidi katika maji ya chumvi (Bahari)
Zaidi ya hayo, mambo kama vile misukosuko, mtiririko mkubwa wa maji, na kuwepo kwa vichafuzi (Water pollution) vinaweza pia kuchangia kutokea kwa povu kubwa katika mto.
HALI ILIVYOKUWA NA ILIVYO MAJIRA YA JIONI.
Maeneo yaliyopata mkusanyiko mkubwa wa mapovu majira ya asubuhi ni: Tubuyu shule, Mfuruni, JKT nanenane, kituo cha mafuta cha ATN, Tungi makaravati, na maegesho na eneo la kuoshea magari jirani na chuo cha Jordan.
Mpaka kufikia majira ya ya Jioni hii; hali hiyo imepungua na kupotea katika baadhi ya maeneo isipokuwa maeneo yenye makoronga na mtiririko wa maji mengi.
MADHARA KWA BINADAMU NA MIFUGO
Mpaka sasa hakuna taarifa ya madhara kwa binadamu na mifugo iliyoripotiwa kutoka na uwepo wa mapovu hayo katika mto na vijito mbalimbali.
ANGALIZO
Kutoka na kutofahamika kwa chanzo halisi Cha mapovu haya, hatua mbalimbali zinapaswa kuchukuliwa na Wanachi pamoja na serikali zetu za mitaa katika maeneo yanayopitiwa na mto huu unaounganishwa na mto Ngerengere
Dalili zifuatazo zitaonekana kwa baadhi ya Wananchi ndani ya masaa 12, Endapo mtu atatumia maji ya kunywa ama kuoshea vyombo na matunda pamoja na matumizi ya samaki (kitoweo) kutoka katika mto na vijito vya mto husika
Dalili Kama;
1. Kuumwa Kichwa kuliko kawaida
2. Macho kuwa mekundu kuliko kawaida
3. Muwasho wa ngozi, koo, na pua (kufukuta)
4. Kujawa mate mdomoni kusiko kawaida
5. Kuumwa tumbo
6. Kichefuchefu
7. Kutapika
8. Kuharisha
Note: hali hii inaweza kuwa imesababishwa na umwagaji/utililishaji wa chemikali (detergent) katika mto.
Aidha, watu wenye magonjwa ya asthma, matatizo ya moyo pamoja upumuaji wanatazamiwa kukumbwa na madhara makubwa zaidi endapo watatumia vitu vilivyo kuwa contaminated
Naomba kuwasilisha
Sgt Benjamin Bandula
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji - MOROGORO
January 22, 2024
Home
Unlabelled
TAARIFA KUHUSU UWEPO WA TAHARUKI KWENYE MTO MAENEO YA TUBUYU MOROGORO
TAARIFA KUHUSU UWEPO WA TAHARUKI KWENYE MTO MAENEO YA TUBUYU MOROGORO
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment