HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 16, 2024

Mshindi BSS kuondoka na milioni 20

 Na Mwandishi Wetu


Fainali za shindano la kusaka vipaji maarufu kama Bongo Star Search (BSS) msimu 14 zinatarajiwa kufanyika Januari 27 Warehouse Dar es Salaam ambapo mshindi ataondoka na sh milioni 20 na kiwanja kutoka EPL.



Akitangaza fainali hizo Dar es Salaam Jana Mkurugenzi wa Benchmark Production Ritha Paulsen alisema kati ya washiriki 500 waliojitokeza awali kufanya  usaili watakaoingia fainali ni sita bora pekee.


Alisema mambo yameiva tayari washiriki sita watachuana ili kupata mshindi mmoja atakayeondoka na fedha na kiwanja (sqm 500) mshindi wa pili sh Milioni tatu na mshindi wa tatu sh milioni moja.


"Msimu huu ulikuwa na faraja sana kwasababu walishiriki wasichana wengi na pia, ulikuwa ngumu kuchagua waliobora kwa kuwa kulikuwa na vipaji vingi,"alisema.


Alisema watu wanaotaka kuwazawadia washiriki wanaowapenda wajitokeze. Awali, washiriki walitoka mikoa ya Arusha, Kigoma, Mwanza na Dar es Salaam.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko na Maudhui wa Startimes David Malisa alisema BSS msimu huu wanahitaji pongezi kwani wamekuwa wakifanya kazi kwa kujitolea kwa kuwa no gharama kubwa.


Alisema fainali hizo zitarushwa mubashara kupitia ST Swahili ili kuwapa nafasi waliko mbali kushuhudia mambo yanavyokwenda.



"Kiingilio cha kawaida sh 15000, VIP 30,000 na VVVIP ni sh 50000. Hivyo kwa wale ambao hawajajiunga na familia ya Startimes wajiunge sasa ili wapate kushuhudia kila kitu,"


Ofisa Sanaa Mwandamizi wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Agustino Makame aliwapongeza benchmark kwa kuwekeza kwenye sekta ya Sanaa na kuibua vipaji vya muziki. 


Pia, aliwapongeza wadhamini mbalimbali wakiongozwa na Startimes waliojitokeza kuwaunga mkono.


"Bongo Star Search wanaibua vipaji ni jukumu letu kuwaendeleza baada ya fainali, niyaombe makampuni yajitokeze kuwashika mkono washindi kuwasaidia kutimiza ndoto zao," alisema. 

No comments:

Post a Comment

Pages