HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 10, 2024

Mama Lishe watakiwa kuwa wabunifu


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma akimkabidhi mshindi wa kwanza katika mashindano ya mapishi ya chakula (mama ntilie) fedha tasilim shilingi laki tano, mashindani hayo yamefanyika leo katika Jumbo la Shauri Moyo, Unguja, ikiwa ni shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.



Na Mwandishi Wetu


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amewashauri wajasiriamali nchini, kuendelea kutumia ubunifu wao wa kupika vyakula mbalimbali kwa ajili ya biashara zao za mama ntilie ili waweze kujikwamua na umasikini.

Kauli hiyo ameitowa wakati akizungumza na wajasiriamali katika uwanja wa urafiki, Jimbo la Shaurimoyo, Unguja katika mashindano ya mapishi ikiwa ni shamrashamra za miaka 60 ya Mapainduzi ya Zanzibar. Mhe Riziki katika yeyete ile inahitaji ubunifu hivyo ni vyema mama ntilie wawe wabunifu katika mapichi mbali mbali katiba biashara ya chakula kwani hatua hiyo itasaidia kuongeza kipato na kujikwamua an umasikini.

Waziri Pembe amewataka wajasiriamali hao kuitumia fursa ya mikopo iliyopo  ikiwa ni juhudi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la  mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ya kuwawekea mazingira wezeshi wajasiriamali kwa nia ya  kufikia malengo waliyojiwekea.

Aidha amesema Oryx Gas na Azania Group, wameamua kwa makusudi kuwasaid wajasiriamali  ili  kuhakikisha wajasiriamali wote nchini wanafanikiwa na wanakuwa mfano wa kuigwa katika kutoa huduma bora za vyakula popote nchini.

Naye Mwakilishi wa Jimbo la Shaurimoyo  ambae pia ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais  Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe.Hamza Hassan Juma, amesifu juhudi zinazofanywa na wajasiriamali wa Jimbo la Shaurimoyo kwa kuonesha ubunifu mkubwa wa vyakula mbalimbali ambao  utawasaidia kutambulika kitaifa na kimataifa.

Kwa upande wake Mwakilishi  kutoka Oryx Gas Bi Anjela Bitungwa amesema wameamua kuwapelekea nishati safi ya kupikia kwa lengo la  kulinda mazingira pamoja na afya kwa wajasiriamali wa jimbo la Shaurimoyo ili kuwaepusha na madhara ya kutumia kuni na mkaa na kuahidi kuendelea kuratibu  kwa kutoa  mitungi ya gesi 200, yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 25.

Naye msimamizi wa biashara ya Azania Group Bw Joel Laiser, amesifu hatua ya maendeleo iliyofikiwa hivi sasa chini ya Rais Dkt Mwinyi katika kuelekea  miaka 60 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, huku akieleza kuwa Azania Group itaendelea kushirikiana na viongozi wa Zanzibar kwa kuwawezesha wajasiriamali kwa kuwapatia nyenzo zote zinazozalishwa katika kampuni hiyo ili kuwasaidia wajasiriamali hao.


Washindi watatu wamepatikana na kupatiwa zawadi,  ambapo mshindi wa kwanza katika mashindano ya mapishi ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar amezawadiwa shilingi laki tano, Mchele, Unga wa Sembe, Unga wa Ngano kilo 50 kilo moja, Sukari  na Mafuta lita 20.

No comments:

Post a Comment

Pages