Maonesho
hayo yamezinduliwa Januari 10, 2024 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi, yakiwa ni sehemu ya Sherehe za
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Maonesho
hayo ambayo yamebeba kauli mbiu isemayo “Biashara Mtandao kwa Maendeleo ya
Biashara na Uwekezaji” yanawashiriki zaidi ya 500 kutoka taasisi mbalimbali za
bara na visiwani, wakiwemo wajasiriamali na yanatarajiwa kufikia kilele Januari
19, 2024.
PSSSF
imetumia fursa hiyo kuwahudumia wananchama wake ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu
ya matumizi ya teknolojia katika kupata huduma za Mfuko, kupitia PSSSF
Kiganjani.
Huduma
hizo ni pamoja na kupata taarifa za Mafao yatolewayo na Mfuko, Taarifa za
Michango, Taarifa za Uwekezaji ikiwa ni pamoja na Wastaafu kujihakiki.
No comments:
Post a Comment