HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 03, 2024

MBUNGE KYOMBO AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA MIRADI MINGI YA MAENDELEO KAGERA

 


Mbunge wa Jimbo la Nkenge Frolent Kyombo akiongeza na Wadau wa maendeleo na Wananchi wa kata ya Ruzinga Wilayani Misenyi katika maadhimisho ya maendeleo ya kata hiyo. 


Na Lydia Lugakila, Misenyi


Mbunge wa Jimbo la Nkenge Wilayani Misenyi Mkoani Kagera Florent Kyombo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyoipambania kata ya Ruzinga na maeneo mbali mbali ya Wilaya hiyo kwa miradi mbali mbali ya maendeleo.


Kyombo ametoa pongezi hizo katika maadhimisho ya siku ya maendeleo ya Kata ya Ruzinga maarufu (Ruzinga Day) yaliyofanyika katika kata hiyo Wilayani Misenyi.


Kyombo amesema  kuwa Rais Samia amefanya kazi kubwa katika Kata hiyo na maeneo mengine ya Wilaya hiyo ambapo miradi mingi na mikubwa ya maendeleo imeonekana ikiwemo miundo mbinu ya Barabara ndani ya kata hiyo ambapo Barabara zimeendelea kufumuliwa, ujenzi wa miundo mbinu ya shule, Afya, Elimu na umeme ambao umekuwepo wa uhakika kasoro Vitongoji vichache ambavyo mpaka sasa juhudi kubwa zinaendelea kufanyika ili umeme upatikane kwa haraka.


Amesema ni kazi ya Wananchi kuhakikisha  miradi hiyo ya maendeleo inatunzwa vizuri kwani Serikali hutumia fedha nyingi katika miradi hiyo.


Aidha Kyombo amewapongeza Wana umoja na wadau wa maendeleo ujulikanao kama Ruzinga Development Association -RD na Wananchi kwa ujumla kwa namna walivyokuwa na hamasa kubwa ya kuchangia shughuli za maendeleo kwa kushirikiana na Serikali kwa kiasi kikubwa kuhakikisha maendeleo yanakuja katika kata hiyo.


"Niwapongeze kwa kuanzisha miradi na Serikali ikifika hatua fulani inamalizia mingine nimefurahi kuona mnachangia kidogo pale Serikali ilipochangia hadi mradi kukamilika hii ni hatua kubwa alisema" Mbunge huyo.


Aidha amesema kuwa Ofisi ya Mbunge itaendelea kutoa ushirikiano kwa umoja huo na kwa Wananchi  wa kata hiyo, Viongozi wa Chama na Serikali ili kuondoa changamoto mbali mbali zilizodumu kwa muda mrefu.


Mbunge huyo amechukua nafasi hiyo kuwaomba watendaji katika sekta ya Elimu kuhakikisha wanaongeza ubunifu katika kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi hii ni baada ya kiwango cha ufaulu kuonekana Kushuka kwa miaka mitatu iliyopita Mkoani Kagera.


Hata hivyo Ameongeza kuwa atahakikisha anaendelea kuwapambania Wananchi katika Jimbo lake ili kubaini kusikiliza na kutatua changamoto zilizopo ili Wananchi waishi bila vikwazo.

No comments:

Post a Comment

Pages