VICTOR MASANGU, KIBAHA
KATIKA
kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan
katika kukuza sekta ya michezo Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry
Koka ametoa vifaa vya michezo ikiwemo jezi 16 na mipira 20 kwa ajili
ya michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 25.
Akikabidhi msaada huo kwa viongozi wa Chama cha soka Wilaya ya Kibaha (KIBAFA) katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji Method Mselewa alibainisha kwamba lengo kubwa la kutoa vifaa hivyo ni kutoa fursa kwa kuonyesha vipaji na kukuza mchezo wa soka.
Katika
halfa hiyo ya makabidhiano ambayo imehudhuriwa na viongozi mbali mbali
wa Kibafa,pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa chama cha mapinduzi
(CCM ) kwa lengo la kushuhudia utekelezaji wa ilani katika nyanja ya
michezo
"Leo
kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini tumekuja kukabidhi vifaa
vya michezo kwa uongozi wa soka Wiaya ya Kibaha na tumetoa mipira 20
pamoja na jezi seti 16 ambazo zimegharimu kiasi cha shilingi milioni
3.5 na zitapewa timu ambazo zitashiriki katika michuano hiyo," alisema
Mselewa.
Aliongeza kuwa
lengo la Mbunge ni kuendea kusaidia vijana wa jimbo lake katika
kuendeleza na kukuza michezo mbali mbali katika kata zote 14 ikiwemo
mchezo wa soka kwa vijana wa Jimbo lake la Kibaha mjini.
Mselewa
katika hatua nyingine alisema kuwa michuano hiyo ambayo mdhamini wake
mkuu ni Mbunge na kwamba wataendelea kushirikiana bega kwa bega na
viongozi wa mpira wa miguu ili kutimiza malengo ya michuano hiyo.
Pia
katika hatua nyingine aliwahimiza wacheza na timu zote kuwa na nidhamu
na kuzingatia sheria na taratibu zote za mashindano ikiwemo kuzingatia
suala la kutozidisha umri.
Kwa
Upande wake Mwenyekiti wa Chama cha soka Wilaya ya Kibaha (KIBAFA)
Robert Munisi amempongeza Mbunge Koka kwa kuweza kuunga jitihada za
serikali katika kukuza sekta ya michezo hususan kwa vijana katika jimbo
lake.
"Kiukweli napenda
kwa dhati kabisa kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Kibaha kwa kuweza
kusaidia sekta ya michezo na amesaidia vifaa hivi kwa lengo la
kufanikisha michuano hii ya vijana wenye umri chini ya miaka 25,"alisema
Munisi.
Naye Kaimu
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji amesema
kwamba kite do alichokifanya Mbunge ni moja kati ya utekelezaji wa ilani
kwa vitendo katika nyanza ya michezo husan kwa vijana.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha soka Wilaya ya Kibaha (KIBAFA) David Mramba
ambaye pia ni Katibu mwenezi wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani
alisema kwamba dhamira ya Mbunge ni kuendeleza vipaji kwa vijana hivyo
ni vema kumuunga mkono kwa dhati.
Mashindano
hayo yaliyopewa jina la Kibafa vijana Cup yanatarajiwa kuanza kutimua
vumbi lake rasmi kuanzia Januari 6 mwaka huu katika kiwanja cha
Mwendapole kwa kuzishirikisha time 16 kutoka Jimbo la Kibaha mjini.
No comments:
Post a Comment