Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Magomeni, Bi. Mary Marungi akibofya kitufe kuchezesha droo ya wiki ya tisa ya Kampeni ya Kuhamasisha Matumizi yasiyo ya pesa taslim 'NMB MastaBata Halipoi' kumtafuta mmoja wa washindi wa droo hiyo, ambapo washindi 100 walijishindia shilingi milioni 10. Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Bw. Rasuli Masoud pamoja na Meneja Huduma za Kadi, Bi. Ednamamu Mshubi.
Mmoja wa wateja wa Benki ya NMB Tawila Magomeni akicheza mchezo wa bahati nasibu ya papo hapo kujishindia ama shilingi 50,000/-, au flana na kofia za NMB iliyochezeshwa sambamba na droo ya wiki ya tisa ya Kampeni ya Kuhamasisha Matumizi yasiyo ya pesa taslim 'NMB MastaBata Halipoi' kumtafuta mmoja wa washindi wa droo hiyo, ambapo washindi 100 walijishindia shilingi milioni 10.
NA MWANDISHI WETU
KAMPENI ya Weka, Tumia ana Ushinde inayoendeshwa na benki ya NMB, ikilenga kuhamasisha matumizi yaisyo ya pesa taslimu, imezidi kuchanja mbuga, baada ya Alhamisi Januari 4 kuchezeshwa kwa droo ya tisa, iliyozalisha washindi 100 waliojinyakulia Sh. Mil. 10 (sawa na Sh. 100,000 kila mmoja).
Idadi ya washindi 100 wa droo hiyo, inafanya wateja wabenki hiyo waliojinyakulia zawadi za wiki kufikia 900 kati ya 1,200 wataonatarajia kujishindia kiasi cha Sh. 100,000 kila mmoja katika kipindi cha miezi mitatu ya kampeni hiyo ijulikanayo kama ‘NMB MastaBata Halipoi,’ iliyozinduliwa Oktoba 27 mwaka jana 2023.
Ukiondoa washindi 1,200 wa kila wiki, NMB MastaBata Halipoi – kampeni yenye zawadi mbalimbali zenye thamani ya Sh. Mil. 350, inatoa pia washindi 30 wa mwisho wa mwezi (washindi 15 kwa kila mwezi wanaojizolea Sh. 500,000 kila mmoja), washindi 240 wa Papo kwa Papo wanaopata Sh. 50,000 kila mmoja.
Akizungumza wakati wa droo hiyo iliyoendeshwa chini ya usimamizi na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Rasuli Masudi, Meneja wa NMB Tawi la Magomeni, ilikochezeshwa droo hiyo, Mary Marungi, alisema wateja wa Papo kwa Papo wanaozawadiwa ni wale watakaokutwa wakifanya manunuzi kwa kadi.
“Pia tunawazawadia washindi 10 na wenza wao ambao wapata fursa ya Kwenda kuhudhuria Tamasha la NMB Full Moon Party linalofanyika Kendwa Rocks Hotel, Zanzibar, safari iliyogjharamiwa kila kitu na NMB, pamoja na kupewa pesa ya matumizi binafsi ya Sh. 200,000 kila mmoja.
“Kampeni hii itahitimishwa kwa washindi 12 na wenza wao kufanya safari ya utalii mjini Cape Town nchini Afrika Kusini, gharama zote zikiwa zimelipiwa na NMB, ambako watakula bata kwa siku tano,” alisema Marungi wakati wa ufunguzi wa droo hiyo iliyoambatana na zawadi kwa wateja waliokuwa wakihudumiwa tawini hapo.
Aidha, Marungi alibainisha kuwa nia ya NMB MastaBata Halipoi ni kuifanya jamii kuendana na kasi ya teknolojia, wanakowapa msisitizo wa kufanya manunuzi na malipo kwa kutumia NMB MasterCard, Lipa Mkononi (QR Code) na Vituo vya Mauzo (PoS) na malipo ya mtandaoni na yale ya kwenye vituo vya mafuta, ‘supermarket’ na migawaha mbalimbali.
Kwa upande wake, Masudi kutoka GBT, aliipongeza NMB kwa kudumisha utamaduni chanya wa kuzawadia wateja wao waliouanza mwaka 2018 ilipozindua kampeni hiyo,na kwamba wateja wa benki hiyo wanapaswa kushiriki matumizi ya kadi ili kujihakikishia nafasi za kushinda peza taslimu na safari za kitalii ndani nan je ya nchi.
“Sisi GBT tunawapongeza NMB kwa hiki inachofanya kwa msimu wa tano sasa, inaonesha namna inavyowajali wateja wao kwa kuwazawadia kila wanapoweka akiba na wanapofanya matumizi. Jukumu letu ni kusimamia na tunawahakikishia wote kwamba droo hizi zinafanyika kwa kufuata vigezo na masharti, hakuna ujanja ujanja,” alibainisha Masudi.
Droo hiyo ya 9 iliyoshuhudiwa pia na Meneja wa Kitengo cha Kadi NMB, Sophia Mwamwitwa na Meneja Huduma za Kadi NMB,Ednamamu Mshubi, imefanyika wiki moja tu tangu wateja 15 walipojinyakulia zawadi ya Sh. 500,000 kila mmoja katika droo ya piliya mwisho wa mwezi iliyofanyika Desemba 29 jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment