Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amesema hali ya
usalama nchini imeendelea kuimarika huku akiwatoa hofu Watanzania juu ya
usalama waona kubainisha kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na
wananchi limefanikiwa kudhibiti ajali na vitendo vya uhalifu
Kauli hiyo Waziri Mhandisi Masauni ameitoa jijini humo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha Watumishi wa Wizara na Jeshi la Polisi.
"Serikali inafanya kila jitihada kuliwezesha jeshi la Polisi na Jeshi linafanya jitihada kubwa kulinda usalama na raia, tukio lolote la kiuharifu hakuna hata moja ambalo hatua hazijachukuliwa na zinaendelea kuchukuliwa wananchi wawe na imani na jeshi lao na Serikali,” amesema Waziri Mhandisi Masauni.
Waziri Mhandisi Masauni amewahakikishia wananchi kwamba hakuna tukio lolote la kihalifu ambalo halitachukuliwa hatua.
“Likiwa linamuhusisha mtu yoyote ambalo halijafanyiwa kazi hata polisi nina documents za matukio yote ambayo yamevuta hisia kwa jamii mlioeleza ndo yale niliyoyategemea kwa faida ya Watanzania," ameongeza Waziri Mhandisi Masauni.
Waziri Masauni amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kulipatia fedha jeshi la polisi zilizosaidia kulifanyia maboresho ikiwemo unuzuzi wa vitendea kazi vya kisasa, mafunzo na masilahi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camilius Wambura, amesema Askari hutumia nguvu katika kukamata wahalifu wakiwemo Panya Road kukiwa na sababu za msingi kinyume na hapo atachukuliwa hatua za kinidhamu.
"Panapotokea Askari akatumia nguvu bila sababu atakua amekwenda kinyume na atachukuliwa hatua za kinidhamu askari anapotumia nguvu inayodhidi nguvu ya mtuhumiwa basi atachukuliwa hatua,” amesema IGP Wambura na kuongeza,
"Panya road hutumia silaha za jadi kufanya uharifu na mara nyingi husababisha vifo, Polisi ni binadamu kama binadamu wengine hatakiwi kufa kizembe ,Nguvu anayotumia askari aliyopo kwenye ground ndio anayepaswa kupima ni namna gani anaweza kutumia nguvu ,Kwaio nguvu ya Panya road ndio inasababisha askari atumie nguvu kumuua,”.
Kuhusu sakata la kuchomwa visu Beatrice Minja, IGP Wambura amesema "Ilikua Taarifa ya kuchomwa visu kituo cha Polisi Tarakea ,alichomwa Visu na mpenzi wake Lucas Tarimo ambae alitoweka kijijini ,Na hakuwahi kupatikana mpaka tarehe ile alipopatikana ,Utorokaji wa mtuhumiwa aliyetoweka ni process na unahitaji utaalmau wa hali ya juu ,Si kweli kwamba mtandao wa kijamii ulifanya tumtafute ila alikua anatafutwa siku zote mpaka pale tulipomkamata.
IGP Wambura amefafanua kuwa wamepeana maelekezo na makamanda ili kuhakikisha jeshi hilo linaendelea kufanya kazi kwa weledi.
No comments:
Post a Comment