Mkazi wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Peter Lipembe(mwenye shati ya bluu)akiwa ameshika hundi baada kujishindia kitita cha Sh250 bilioni kutoka kampuni ya michezo ya kubashiri ya BetwayTanzania.
Mwandishi Wetu
Mkazi wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Peter L. amejishindia kitita cha milioni 250 kutoka kampuni ya michezo ya kubashiri ya Betway Tanzania.
Peter anakuwa mshindi wa pili kutoka mkoani humo baada ya Bernard M. aliyejinyakulia ushindi kama huo Disemba 2023.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi yenye kiasi hicho cha fedha katika hafla iliyofanyika katika Ofisi za Betway Tanzania jijini Dar es Salaam, Peter L. amesema “Imekuwa kama ndoto kupata kiasi hicho cha fedha kwenye siku yangu yakuzaliwa”, ambacho anadai hakutegemea hata siku moja kama angeweza kuja kuwa mshindi na kuingia katika kundi la matajiri nchini huku akiwasisitiza wananchi wengine kushiriki katika kubashiri na michezo mingine inayoendeshwa kupitia kampuni hiyo ya Betway Tanzania.
Aidha, mshindi huyo ameushukuru uongozi mzima wa kampunihoyo kwa ushirikiano waliuonyesha tangu alipotangazwa kuwa mshindi hadi hatua ya kukabidhiwa fedha zake huku akisisitiza kuwa ataendelea kubashiri zaidi na zaidi kupitia kampuni hiyo kwa kuwa inaaminika.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Betway Tanzania, Calvin Mhina, mbali na kumpongeza mshindi huyo amesema kampuni hiyo imekuwa karibu na wateja wake wakati wote huku akisisitiza kuwa ushindi na malipo kwa mshindi huyo ni kielelezo cha uaminifu wa kampuni hìyo.
"Sisi kama kampuni bora ya michezo ya kubashiri Tanzania na Duniani kote ushindi huo unatufanya kuendelea kujiweka mbele zaidi hasa kwa kuwa na promosheni nyingi nzuri zinazomuwezesha mtu kushinda kwa urahisi,"amesema Mhina.
No comments:
Post a Comment