VICTOR MASANGU, KIBAHA
Katibu
wa Chama cha malinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Issack Kalleiya
kuchangamkia fursa ya kujitokeza kwa wingi katika kuchukua fomu kwa
ajili ya kugombea nafasi ya udiwani wa kata ya Msangani ambayo ipo wazi
kwa sasa.
Katibu
huyo aliwahimiza wanachama wote ambao wana sifa za kugombea kujitokeza
bila woga kwa lengo la kuweza kuziba nafasi hiyo ya diwani ambayo ipo
wazi kutokana na aliyekuwa diwani wa kata hiyo kufariki dunia hivi
karibuni.
Katibu
Kalleiya aliyasema hayo wakati akizungumza na wajumbe wa Halmashauri
Kuu ya Kata Msangani kuwa uchukuaji wa fomu ndani ya Chama utaanza
tarehe 21/02/2024 hadi 23/02/2024 ambapo wanachama wote wenye sifa za
kugombea watatakiwa kuchukua fomu na kurudisha ndani ya muda uliopangwa.
Amesema,
Ofisi ya CCM Wilaya itakuwepo katika kuhakikisha kila mwanachama
aliyechukua fomu anapata nafasi ya kuirudisha ili kusije kutokea
malalamiko ya wagombea kukuta Ofisi za Kata zimefungwa.
Kalleiya
alisema kwamba zoezi hilo lonapaswa lifanyike kwa uweledi na
kusisitika kuwa hatopependa kusikia mwanachama yoyote ameshindwa
kuchukua fomu yq Ugombea, bali kila mwenye sifa achukue ila maamuzi ya
nani anafaa yatakuwa ni maamuzi ya Halmashauri Kuu ya Kata.
Pia,
Katibu wa CCM amesisitiza kuhusu uundwaji wa Kamati za Ushindi katika
kila Tawi na Mashina ili kuhakilisha Chama Cha Mapinduzi kinashinda
nafasi hiyo kwa mara nyingine tena.
Akizungumzia
suala la daftari la wapiga kura, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha
Mjini Ndg Mwl. Mwajuma Nyamka amesmea uchaguzi huu mdogo ni ww kujaza
nafasi baada ya Diwani wa Kata ya Msangani kufariki ila kiutaratibu wale
ambao walipiga kura katika Uchaguzi wa mwaka 2020 ndiyo wanapaswa
kupiga kura.
Akifafanua
zaidi, Mwenyekiti amesema kwa wale ambao wametimiza umri wa kupiga kura
na hawakuwepo katika daftari la wapiga kura la mwaka 2020 hawataruhusiwa
kushiriki Uchaguzi huu.
Aidha,
Kamati ya Siasa Wilaya iliweza kufanya ziara katika Matawi kila mmoja
akiwa mlezi wa tawi na kusikiliza mawazo na ushauri wa wanachama ili
kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo na kipi kifanyike na kuweza
kupata ushindi wa kishindo.
Tume
ya Uchaguzi nchini imetangaza tarehe ya Uchaguzi wa kujaza nafasi za
Udiwani nchini ambapo Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe
20/03/2024.
No comments:
Post a Comment