NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Uongozi
wa chama cha soka Mkoa wa Pwani (COREFA) pamoja na chama cha soka
Wilaya ya Kibaha (KIBAFA) umempongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini
Silvestry Koka kwa kuamua kujitoa kwa hali na mali kusapoti sekta ya
michezo hasa kwa vijana.
Akizungungumza
wakati wa halfa ya kufunga rasmi mashindano ya Kibafa Vijana Cup chini
ya umri wa miaka 25,Makamu Mwenyekiti wa Corefa Mohamed Lacha alisema
kwamba mbunge Koka ameweza kusapoti michuano hiyo kwa asilimia mia moja.
Lacha
alisema kwamba amefarijika sana kuona sapoti kubwa ambayo ameweza
kuitoa mbunge huyo kwa lengo la kuweza kufanikisha mashindano hayo ya
vijana yaweze kufanyika na kwamba yamefanikiwa.
"Kwa
kweli mimi kwa nafasi yangu kama Makamu mwenyekiti wa Corefa nipende
kwa dhati kabisa kumshukuru Mbunge wa Jimbo la kibaha kwa kutoa fedha
kwa ajili ya kudhamini mashindano haya,"alisema Lacha
Kadhalika
aliongeza kuwa kauli mbiu yao kubwa ni kwamba mpira lazima uchezwe
katika Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa mchezo wa
soka.
"Tunashukuru
mashindano haya yamemalizika salama na timu zote zimeweza kupatiwa
zawadi zao ambazo zimetolewa na mdhamini mkuu ambaye ni Mbunge wa Jimbo
la Kibaha mjini Silvestry Koka,"alifafanua Lacha.
Kwa
upande wake .mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya chama cha soka Wilaya
ya Kibaha (KIBAFA) Jeremia Komba alisema kwamba Mbunge huyo amekuwa
mstari wa mbele katika kushiriki kikamilifu katika kusaidia sekta ya
michezo.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya mji Kibaha Mussa Ndomba aliwataka viongozi wa vyama soka
kuendelea kumpa sapoti Mbunge huyo kwani ameweza kutumia zaidi ya
milioni sita katika kudhamini michuano hiyo.
Pia
na sisi kama halmashauri tumejipanga vilivyo katika kutenga maeneo ya
viwanja kwa michezo ili kuweza kutoa fursa zaidi ya vijana kupata ajira
kupitia michezo.
Nao
baadhi ya wachezaji na wadau wa mchezo wa kabumbu walisema jambo ambalo
amelifanya Mbunge Koka la kudhamini michuano hiyo kwa asilimia 100
linatia moyo katika nyanja ya kukuza mchezo wa soka hasa kwa vijana.
Waliongeza
kuwa kitendo ambacho amekifanya Mbunge Koka cha kuziwezesha timu 16 kwa
kuzipatia jezi pamoja na mipira ikiwemo na kutoa zawadi kwa washindi
watatu kimewapa faraja sana katika medani ya soka.
Mbunge
wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amekuwa ni nguzo kubwa ya
kuwasaidia vijana katika kuibua na kukuza vipaji walivyonavyo ambapo
safari hii amekuwa mdhamini mkuu wa michuano ya Kibafa vijana Cup kwa
asilimia mia moja.
No comments:
Post a Comment