Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (VPO), Bi Mary Maganga, ameipongeza Hospitali ya Benjamin Mkapa(BMH) kwa huduma bora za afya.
Katibu Mkuu ameyasema haya leo jijini Dodoma wakati alipokutana na uongozi wa Hospitali hii ya umma inayohudumia Kanda ya Kati na mikoa ya jirani.
"Tumekuwa tukipata huduma hapo kwenu (BMH) na tunapata huduma nzuri tu pasipo kujieleza kuwa tunatoka ofisi gani," amesema Katibu Mkuu.
Uongozi wa BMH uliomtembelea Katibu Mkuu ofisini kwake, Mtumba mji wa Serikali, umeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali, Dkt Alphonce Chandika
Bi Mary pia ameipongeza Hospitali hii ya Rufaa ya Kanda kwa kutunza mazingira vizuri.
"Nawapongeza kwa kutunza mazingira ya Hospitali vizuri. Ni taasisi ya umma ambayo imepanda miti mingi pia majiko ya kantini zenu hamtumii majiko ya mkaa," amesema Katibu.
No comments:
Post a Comment