THAMANI ya uwekezaji katika Taasisi zinazo simamiwa na ofisi ya Msajili na Hazina yameongezeka kutoka Shilingi Trilioni 70 katika kipindi cha mwaka 2021 hadi kufikia Shilingi Trilioni 76 mwaka 2023 sawa na ongezeko la 8.6%.
Yamesemwa leo na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Mobhare Matinyi Machi 24 2023 alipozungumza na wahariri na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
"Serikali imeongeza umiliki wa hisa katika Kampuni ya Almasi ya Williamso Diamonds kutoka 25%hadi 37%huku ikisaini mikataba ya ubia wa 16% zisizohamishika katika Kampuni za madini"amesema Matinyi.
"Katika kipindi cha kuanzia Machi 2024 hadi Februari 2024 Wizara ya Madini imefanikiwa kujiendeleza sekta kwa namna mbalimbali ikiwemo kukusanya maduhuli na kufikisha kiasi cha Shilingi Trilioni 1.93 awali mwaka 2021/22 ilikuwa Shilingi. Bilioni 591.5 lakini hadi kufikia 2023/24 imefikia Shilingi Bilioni 690.4.
Aidha Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi, amesema kuwa Tanzania imeendelea kuwa katika kundi la nchi zenye uchumi wa pato la kati ikimaanisha pato la wastani la kila mwanachi kwa mwaka (GNI per capital) ambapo ingawa mwaka 2019 ilikuwa kiasi cha dola 1,080 (Tsh. 2,743,813) lakini mwaka 2022 ni dola 1,200 ( Tsh. 3,048,681).
“Uchumi wa Tanzania umeendelea kukua licha ya athari kubwa za mripuko wa UVIKO-19 duniani pamoja na vita za Urusi na Ukraine na pia katika nchi za Mashariki ya Kati matatizo haya yaliutikisa uchumi wa dunia na Tanzania ambao ulikuwa umefikia wastani wa ukuaji wa zaidi ya 7% na kuushusha hadi 4.2% mwaka 2020" amesema.
“Hata hivyo, hivi sasa ukuaji umefikia 5.2% kutokana na uongozi thabiti wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Sukuhu Hassan, aidha Tanzania imeendelea kuwa katika kundi la nchi zenye uchumi wa pato la kati, ikimaanisha pato la wastani la kila mwanachi kwa mwaka (GNI per capital) ambapo ingawa mwaka 2019 ilikuwa kiasi cha dola 1,080 (Tsh. 2,743,813) lakini mwaka 2022 ni dola 1,200 ( Tsh. 3,048,681)".
“Serikali imeendelea kudhibiti mfumuko wa bei ambapo kwa sasa ni chini ya 4% - kiwango ambacho ni miongoni mwa viwango bora katika nchi za jumuiya za kikanda ambazo Tanzania ni mwanachama, kama Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)”amesema Matinyi.
“Akiba ya fedha za kigeni imeendelea kuwa toshelezi ambapo katika kipindi chote cha miaka mitatu hadi Desemba 2023, nchi ilikuwa na akiba inayotosha kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kwa miezi 4.5, ikiwa ni kiwango cha juu ya lengo la miezi 4, akiba hiyo ni sawa na dola za Marekani bilioni 5.4”
No comments:
Post a Comment