HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 28, 2024

AZAM WAPEPEA CAF CL, MNYAMA HOI

Na John Richard Marwa

Klabu ya Azam FC imeungana na Mabingwa Young Africans SC katika kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL msimu ujao mara baaaa ya kumaliza nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa dhidi ya Simba SC.


Azam wamepata ushindi wa mabao 2-0 kama ambavyo Simba wameshinda dhidi ya JKT Tanzania kwenye michezo ya mwisho ya kuhitimisha msimu iliyomaliza jioni ya leo.

Kwa matokeo hayo Azam FC wamefikisha pointi 69 sawa na Simba huku wakiwa wamefunga mabao 63 dhidi ya 59 waliyofunga Simba huku Simba wakiwa wameruhusu mabao 25 dhidi ya 21 waliyofungwa Azam FC.

Kwa matokeo hayo ya leo Young Africans ni bingwa akiwa na pointi 80 baada ya kuwafunga Tanzania Prisons mabao 4-1. Azam FC nafasi ya pili, Simba nafasi ya tatu huku Coastal Union wakifunga nne bora. Timu zote nne zina tiketi ya kushiriki mashindano ya Kimataifa msimu ujao.

Matokeo mengine kwenye michezo mingine ni Coastal Union dhidi ya KMC FC ni suluhu. Mashujaa wameshinda mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC, Ihefu wamewatwanga Mtibwa Sugar mabao 4-1.

No comments:

Post a Comment

Pages