HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 28, 2024

KWEHERI NBC PL 2023/2024 TULIKUPENDA SANA

Na John Richard Marwa

Tamati ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NBC PL msimu wa 2023/2024 unafika mwisho leo kwa michezo nane kupigwa katika Viwanja nane ambapo kila timu inahitimisha mchezo wake wa 30.

Mabingwa Young Africans SC wako Azam Complex Chamazi kuwavaa wajelajela Tanzania Prisons, Yanga was pointi 77 na kama leo watapa alama tatu wataumaliza msimu wakiwa na pointi 80 huku kiu yao kubwa ni kuona kiungo wao Stephanie Aziz Ki akifunga na kutwaa kiatu cha dhahabu.


Vita ya nafasi ya pili bado ni ya moto ambapo Geita Gold FC wakiwa nyumbani Nyankumbu wanakibarua cha kusaka ushindi ili kupata nafasi ya kutafuta nafasi ya kusali Ligi Kuu msimu ujao huku Azam FC wao wakihitaji pointi tatu zitakazo wapa nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL msimu ujao.

Kimbembe kingine kitakuwa Dimba la Benjamin Mkapa ambapo Mnyama Simba anawakabili JKT Tanzania, wekundu  wa Msimbazi hakuna wanachohitaji zaidi ya pointi tatu na mabao ya kutosha ili kuweza kumshusha Azam FC nafasi ya tatu na wao kupanda  nafasi ya pili itakayowarejesha kwenye maisha yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL msimu ujao.

Michezo mingine itakayopigwa ni kule Majaliwa Stadium ambapo wenyeji Namungo FC wanawakaribisha Tabora United ambao wanahitaji ushindi kujihakikishia nafasi ya kusali Ligi Kuu msimu ujao.

Pale Liti Singida, Ihefu FC ama Singida Black Stars wao wanakipiga dhidi ya Mtibwa Sugar ambao tayali wanajiandaa na maisha ya Championship.

Mwisho wa reli Kigoma wenyeji Klabu ya Mashujaa wao wanamaliza msimu dhidi ya Dodoma Jiji FC katika Dimba la Lake Tanganyika.

Katika Jiji la waja leo kuondoka majaliwa Wagosi wa Ndima Coastal Union wanakitwanga dhidi ya KMC FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Mchezo mwingine ni kati ya Kagera Sugar dhidi ya Singida Fountain Gate FC. Michezo yote ikipiga majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.


No comments:

Post a Comment

Pages