MABADILIKO
ya Sheria ya Madini ya mwaka 2010 yametoa fursa ya kuboresha mazingira
ya uwekezaji nchini na kuhakikisha watanzania wananufaika na rasilimali
madini.
Hayo yamesemwa leo Mei 22, 2024 na Waziri wa Madini.
Mhe. Anthony Mavunde katika ufunguzi wa Jukwaa la Tatu la Ushirikishwaji
wa Watanzania katika Sekta ya Madini linaloendelea kwenye Ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano AICC jijini Arusha.
Waziri Mavunde amesema
kuwa, katika mabadiliko hayo suala la Ushirikishwaji wa Watanzania
limepewa kipaumbele ili kuhakikisha wawekezaji wote wanaojihusisha
katika mnyororo wa uzalishaji na biashara ya Madini wanatoa kipaumbele
kwa Watanzania.
“Marekebisho ya mwaka 2017 ya Sheria ya Madini,
yalipelekea kutungwa kwa Kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania za Mwaka
2018 ili kuweka usimamizi thabiti katika utekelezaji wa masuala ya
Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini nchini,” amesema
Mhe. Mavunde na kuongeza,
“Kulikuwa na malalamiko mengi,
watanzania walikuwa ndugu watazamaji mpaka vyakula vilikuwa vinatoka
nje, lakini baada ya mabadiliko ya sheria ya mwaka 2017 ushirikishwaji
wa watanzania umekuwa mkubwa sana sambamba na watanzania kushika nafasi
za juu za uongozi kwenye kampuni za madini,”amesema Mhe. Mavunde.
Amesema
kuwa, katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Machi, 2024, Wizara kupitia
Tume ya Madini ilipokea na kupitia jumla ya mipango 801 ya
Ushirikishwaji wa Watanzania katika shughuli za Madini sawa na ongezeko
la asilimia 57 ikilinganishwa na mipango 510 iliyopokelewa katika
kipindi kama hicho kwa Mwaka wa Fedha uliopita.
“Hii ni wazi
kuwa mwamko wa Watanzania katika kushiriki fursa zilizopo kwenye Sekta
ya Madini unakua kwa kasi,”amesema Mhe. Mavunde.
Amesema kuwa
Wizara kupitia Tume ya Madini imeendelea kuhakikisha kuwa Watanzania
wanapatiwa kipaumbele katika fursa za ajira zinazozalishwa katika migodi
mikubwa na ya kati ya uchimbaji madini hapa nchini.
Ameendelea
kusema kuwa hadi kufikia Machi, 2024 jumla ya ajira rasmi 19,358
zilizalishwa katika migodi hiyo ambapo ajira 18,853 sawa na asilimia 97
zilitolewa kwa Watanzania na ajira 505 sawa na asilimia 3 zilitolewa kwa
wageni.
Pia amesema kuwa ajira kwa watanzania kwenye migodi
zitaendelea kuongezeka ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Madini Sura 123
na Kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania za Mwaka 2018.
Aidha,
amesema kuwa Wizara kupitia Tume ya Madini imeendelea kusimamia ununuzi
wa bidhaa na huduma kwa kuhakikisha kipaumbele kinatolewa kwa
watanzania kwa mujibu wa Sheria ya Madini Sura ya 123.
Amesema,
usimamizi huo umekuwa na matokeo chanya kwa kuongeza idadi ya watanzania
wanaotoa huduma na kuuza bidhaa kuanzia migodi ya uchimbaji mdogo, ya
kati hadi ya uchimbaji mkubwa wa madini nchini.
“Katika Mwaka
2023 kampuni za kitanzania ziliuza bidhaa na huduma migodini zenye
thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.48 ambayo ni sawa na asilimia 90
ya mauzo yote yaliyofanyika migodini yenye thamani ya Dola za Marekani
bilioni 1.65,”amesisitiza Mhe. Mavunde.
Amehitimisha kwa kusema
kuwa, mauzo hayo yaliyofanywa na kampuni za kitanzania kwa mwaka 2023
yalikuwa ni zaidi ya mauzo yaliyofanywa mwaka 2022 ambayo yalikuwa na
thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.08 sawa na asilimia 86 ya mauzo
yote ya Dola za Marekani bilioni 1.26.
May 22, 2024
Home
Unlabelled
Mabadiliko ya Sheria ya Madini yawabeba Watanzania - Mavunde
Mabadiliko ya Sheria ya Madini yawabeba Watanzania - Mavunde
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment