HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 20, 2024

CAMFED TANZANIA YATOA ELIMU YA STADI ZA MAISHA KWA WANAFUNZI GEITA

Mwezeshaji wa Shirika la CAMFED Tanzania, Bi. Ashura Hamis akigawa vitabu vya ‘Progamu ya Dunia Yangu Bora’ kwa Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Sekondari Bung’wangoko mara baada ya kufundisha wanafunzi juu ya programu hiyo.

Wawezeshaji wa Shirika la CAMFED Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Sekondari ya Bung’wangoko mara baada ya kutoa elimu na vitabu vya ‘Progamu ya Dunia Yangu Bora’ walipotembelea shuleni hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Juma la Elimu lililofanyika Mkoa wa Geita hivi karibuni.

Mwezeshaji wa Shirika la CAMFED Tanzania, akiwafundisha wanafunzi wa Sekondari ya Fadhili Bucha juu ya ‘Progamu ya Dunia Yangu Bora’ walipotembelea shuleni hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Juma la Elimu lililofanyika Mkoa wa Geita hivi karibuni.

Wawezeshaji wa Shirika la CAMFED Tanzania, wakimkabidhi vitabu mwalim mkuu wa Sekondari ya Fadhili Bucha mara baada ya kutoa elimu juu ya ‘Progamu ya Dunia Yangu Bora’ walipotembelea shuleni hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Juma la Elimu lililofanyika Mkoa wa Geita hivi karibuni.

Wawezeshaji wa Shirika la CAMFED Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Fadhili Bucha mara baada ya kutoa elimu na vitabu vya ‘Progamu ya Dunia Yangu Bora’ walipotembelea shuleni hapo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Juma la Elimu lililofanyika Mkoa wa Geita hivi karibuni.

SHIRIKA la CAMFED Tanzania limegawa vitabu pamoja na kutoa elimu na mwongozo kwa wanafunzi juu ya stadi za maisha, kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari Mgusu, Bung’wangoko pamoja na Shule ya Sekondari Fadhili Bucha zilizopo mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Juma la Elimu kwa Mwaka 2024, lililomalizika hivi karibuni mkoani  Geita.

Akizungumza katika tukio hilo. Mwezeshaji wa Shirika la CAMFED Tanzania, Bi. Ashura Hamis alisema elimu ya Stadi za maisha wanaoitoa itawasaidia wanafunzi kupata mwongozo juu ya stadi za maisha, hasa kwa kidato cha kwanza na cha pili kujisaidia kujitambua, wao ni nani na wanatakiwa kufanya nini, ili kuweza kufikia malengo yao waliojiwekea.

Akifafanua Zaidi alisema mbali na kutoa elimu hiyo kwa makundi hayo ya wanafunzi wameamua kugawa vitabu kwa walimu wakuu ili kuendeleza ‘Progamu ya Dunia Yangu Bora’ inayofundisha stadi za maisha kwa wanafunzi, ujuzi unaoendelea kuwasaidia na hatimaye kutimiza malengo waliojiwekea.

“…Hivi vitabu tumevigawa dhumuni lake kubwa ni kutoa elimu na mwongozo kwa wanafunzi juu ya stadi za maisha, hata maka shule hizi hazijafikiwa na mradi, wanafunzi wananufaika zaidi na stadi za maisha, wanapata mwongozo wa nini wazingatie kipindi hiki,” alisema, Bi. Ashura Hamis akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Akizungumzia ‘Progamu ya Dunia Yangu Bora’, Bi. Hamis alibainisha kuwa takribani wanafunzi 70,302 kutoka katika shule za sekondari mbalimbali nchini Tanzania wamenufaika na progamu hiyo inayofundisha stadi za maisha kwa wanafunzi hasa, kidato cha kwanza na cha pili, programu inayoratibiwa na Shirika la CAMFED Tanzania.

Kwa Tanzania nzima takribani shule 493 ambazo zinatoka katika mikoa 10 nchini, zinanufaika na elimu hiyo, huku zikiwa na wanafunzi wa kike 37,925 na wanafunzi wa kiume 32,377. Nia na madhumuni ya mradi ni kuwasaidia wanafunzi walioko shuleni kujisaidia kujitambua, kujijua wao ni nani na wanatakiwa kufanya nini, ili kuweza kufikia malengo yao.

"....mpango huu pia unasaidia wanafunzi hao kuweza kumaliza masomo yao, kuwafuatilia wanafunzi walioacha shule kuwashauri na kuwatia moyo ili warejee shuleni na kuendelea na masomo yao, wawezeshaji wa wanafunzi katika mradi huo hawaishii shuleni pekee lakini hata kuwasaidia kiushauri na mwongozo wasichana wanaopata changamoto mbalimbali katika jamii."

No comments:

Post a Comment

Pages